November 26, 2012

Mwanamzuki Lady Jaydee akiwa katika nguo maalum za Diary

PICHA ZA PARTY YA DIARY YA LADY JAYDEE


Kabila awa mbogo ,ataka M23 waondoke Goma


Kabila ataka M23 waondoke Goma

 

Serikali ya Jamhuri ya Demokrasi ya Congo inasema haitazungumza na wapiganaji wa M23 hadi waondoke mji wa Goma ambao waliuteka juma lilopita.
Wanajeshi wa serikali kabla ya mji wa Goma kutekwa
Taarifa hiyo imetolewa siku moja baada ya mkutano wa viongozi wa Maziwa Makuu mjini Kampala, Uganda, kuwasihi wapiganaji waondoke Goma.
Msemaji wa wapiganaji, Kasisi Jean-Marie Runiga, alisema wapiganaji wataondoka Goma baada ya mazungumzo ya amani lakini siyo kabla.
Rais Joseph Kabila wa Congo alikutana na wawakilishi wa wapiganaji mjini Kampala Jumamosi.
Wakuu wa Uganda wanasema yamekuwapo mawasiliano baina ya pande hizo mbili.

November 21, 2012

Helikopta za Umoja wa Mataifa zashambulia wapiganaji Congo

Jeshi la MONUSCO laingia kati Goma

 
Mpiganaji wa M23 kaskazini ya Goma
Helikopta zenye silaha za Umoja wa Mataifa zimeshambulia maeneo ya wapiganaji mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, huku mapambano yanaendelea baina ya jeshi la Congo na kundi la wapiganaji wa M23.
Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kuweka amani, Monusco, kimesema kuwa vikosi vya jeshi la serikali kaskazini ya mji wa Goma, vilishambuliwa Jumamosi asubuhi, na kufanya raia kulikimbia eneo hilo na helikopta za Umoja wa Mataifa kutumwa huko.
Monusco ina idhini ya kuwalinda raia na kuwasaidia wanajeshi wa serikali ikihitajika.
Hakuna idadi iliyotolewa ya maafa yaliyotokea.
Umoja wa Mataifa unazilaumu Rwanda na Uganda kwamba zinawaunga mkono wapiganaji - tuhuma ambazo nchi hizo inakanusha.

Wabunge wa Tanzania wajipanga kupambana na Kenya


BUNGE FC YAJICHUA VILIVYO KWA AJILI YA MASHINDANO YA MABUNGE YATAKAYOFANYIKA NCHINI KENYA



Picha ikionyesha naibu waziri wa elimu Tamisemi Kassimu Majaliwa ambaye ni kocha wa timu ya Bunge FC akiwapa somo wachezaji wakati wa mazoezi katika uwanja wa kumbukumbu ya sheikh amri abeid

November 18, 2012

Mlipuko Nairobi wazua kizaa,wasababisha fujo

Mripuko Nairobi wazusha fujo

 
Watu  wanakadriwa  watano wamekufa katika mripuko kwenye mtaa wa Eastleigh wa Nairobi wenye wakaazi wengi wa Kisomali.
Mwenye duka wa Eastleigh, Nairobi
Shambulio lililenga basi la "matatu" lilokuwa likitoka kati ya mji.
Naibu msemaji wa polisi wa Kenya, Charles Owino, alieleza kuwa bomu liliripuka ndani ya basi lilipokuwa likipita mtaa wa Eastleigh.
Dakika chache baadae vijana waliokuwa na hasira waliwalenga watu wa jamii ya Kisomali kwenye mtaa huo.
Mtu aliyeshuhudia tukio hilo aliiambia BBC kwamba aliona makundi ya Wasomali wakijipanga kupambana na vijana hao ambao walikuwa wakivamia nyumba zao.
Polisi ilibidi kufyatua risasi hewani kuwatawanya watu.
Hili ni shambulio la karibuni kabisa katika miji ya Kenya tangu jeshi la nchi hiyo kuingia Somalia mwaka jana.

Babati wanufaika na Kilimo cha Migomba

Kilimo cha Umwagiliaji Babati cha komboa wakulima ,wanufaika na lishe na kipato

November 17, 2012

Askofu awajia juu wasomi wa Chuo Kikuu Tumaini Makumira










ASKOFU Mkuu wa Kanisa la  Kilutheri Tanzania ,Alex Malasusa amesema  kuwa Chuo Kikuu Tumaini kimelenga kuwaandaa viongozi  na wasomi bora watakaosaidia kuleta maendeleo ya nchi,na kuwa suala la maadili linatiliwa  mkazo .

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kuwatunuku vyeti wahitimu 470 wa shahada mbali mbali waliomaliza chuoni hapo anasema kuwa maadili yanaendana na mavazi na kuwa zoezi la kuwashughulikia wanafunzi wanaovyaa nguo zinazowadhalilisha linaendelea ,na kuwa Uongozi wa vyuo hivyo umelivalia njuga .

Askofu Malasusa anasema kuwa inajukumu lakuunga mkono jitihada za Chuo hicho kwa kuhakikisha kuwa wanaonya watoto wao kuacha kuvaa mavazi ambayo siyo rasmi na kueleza kuwa jukumu la kuwalea watoto na wanafunzi linatakiwa kuanzia katika jamii na familia .

Libya kwa fukuta ,Waziri wa Usalama ajiuzulu

Waziri wa usalama wa Libya ajiuzulu

 
Ripoti kutoka Libya zinaeleza kuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Fawzi Abdel A'al, amejiuzulu.
Magari yaliyoharibika kwenye bomu Triooli, tarehe 19 Agosti
Pichani ni mji wa Libya
Hakujatolewa sababu.
Inatokea siku moja baada ya polisi katika mji mkuu, Tripoli, kutuhumiwa kuwa hawakufanya kitu kuwazuwia Waislamu wa msimam

November 11, 2012

Mazingira bora ya kazi kiini cha Maendeleo,Manyara

Jengo la Utawala  Mkoa wa Manyara ,miongoni mwa majengo bora  ya Serikali hapa nchini ,yaliyopo pembezoni,picha na Mary Mwita

Maendeleo Kiteto yachangiwa na mfuko wa Maendeleo TASAF

Wananchi Kiteto ,wakiwa katika ukarabati wa Barabara ,Kiteto wasifu  msaada wa TASAFAdd caption

WIZARA YATAKA RIPOTI MGOGORO BAGAMOYOSEKONDARI

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imeingilia kati mgogoro ulioibuka katika Shule ya Sekondari ya Bagamoyo kwa kuagiza viongozi wa Idara ya Elimu ya Wilaya ya Bagamoyo kupeleka ripoti kuhusu chimbuko la migogo hiyo ili wizara iweze kuchukua hatua haraka.
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Phillipo Mulugo, Mulugo alisema baada ya wizara yake kupata taarifa za mgogoro imechukua hatua ya kumwagiza Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Bagamoto kupeleka taarifa za chanzo ili hatua zichukuliwe haraka.
Jumatatu wiki hii Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza, alitangaza kuifunga shule hiyo kwa kipindi kisichojulikana kutokana na mgogoro wa kidini katika shule hiyo ambao upelekea amani kutoweka.
Mahiza alisema amechukua uamuzi huo ili kuiwezesha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kutafuta ufumbuzi wa migogoro, utoro wa walimu na kudumisha amani katika shule hiyo.
“Baada ya kufika nimebaini bado kuna tatizo, kwani hadi nafika jana (juzi) nimekuta wanafunzi 356 kati ya 740 walioandikishwa katika shule hiyo hawajulikani walipo na Mkuu wa Shule hajui walipo,” alisema Mahiza.
Hata hivyo, taarifa ambazo NIPASHE ilizipata toka shule hapo zinaeleza kuwa kufungwa kwa shule hiyo kulifuatia wanafunzi tisa kuandikiwa barua ya kusimamishwa masomo, maamuzi ambayo yaliamriwa na Bodi ya Shule hiyo, lakini wanafunzi hao walikataa kuzipokea barua hizo.
Baada ya wanafunzi hao kukataa kuzipokea barua hizo, kulizuka vurugu za wanafunzi shule hapo ambao walikuwa wakiwaunga mkono wanafunzi walioandikiwa barua hizo na hivyo serikali ya mkoa kuchukua hatua ya kuifunga shule kwa muda usiojulikana.

November 10, 2012

Elimu ya Wanafunzi ,Kiteto wakombolewa

Wanafunzi Kiteto wafurahia mazingira bora ya taaluma ,Washukuru TASAF

Wazee wakombolewa na Mradi wa TASAF Babati

Wazee wa Babati wakieleza manufaa  ys ufugsji Nyuki kwa Mwandishi wa Habari Mary Mwita ,waeleza kuupa umaskini Kisogo

CIA director David Petraeus resigns over affair

CIA Director David Petraeus, testifies before the US Senate Intelligence Committee during a full committee hearing on "World Wide Threats." in this 31 January 2012 David Petraeus retired from 37 years in the military to become CIA director

Related Stories

CIA director David Petraeus has resigned from his post, admitting he had an extra-marital affair.
In a statement, Mr Petraeus said he had submitted his resignation to President Barack Obama, and that he had shown "extremely poor judgement".
He described his behaviour as "unacceptable" for the leader of the nation's main intelligence agency.
Mr Petraeus became CIA boss in 2011 after heading international forces in Iraq, then in Afghanistan.
He was the highest-profile military officer of the post-9/11 years, winning plaudits for his role running the "surge" in Iraq and implementing a counter-insurgency strategy in Afghanistan.
'Great patriot' Mr Petraeus' resignation came just three days after President Barack Obama's re-election, and prompted a flurry of statements from the White House, intelligence community and Mr Petraeus himself.
Announcing his decision to stand down, the former general was full of contrition

“Start Quote

By any measure, through his lifetime of service David Petraeus has made our country safer and stronger”
Barack Obama US President
"After being married for over 37 years, I showed extremely poor judgment by engaging in an extra-marital affair," Mr Petraeus said in a statement.
"Such behaviour is unacceptable, both as a husband and as the leader of an organisation such as ours. This afternoon, the president graciously accepted my resignation."
Mr Obama's statement said Mr Petraeus had "provided extraordinary service to the United States for decades", citing both his time as CIA director and service to the military.
"By any measure, through his lifetime of service David Petraeus has made our country safer and stronger."
"Going forward, my thoughts and prayers are with Dave and Holly Petraeus, who has done so much to help military families through her own work."
James Clapper, director of national intelligence, thanked Mr Petraeus for his decades of service: "Dave's decision to step down represents the loss of one of our nation's most respected public servants,"

David Petraeus: Career highlights

  • Graduated from West Point in 1974
  • Commander of Multinational Force Iraq, Feb 2007 to Sept 2008
  • Commander of International Security Assistance Force (Isaf) in Afghanistan, July 2010 to July 2011
  • Became CIA director in Sept 2011 after being confirmed by the senate 94-0
"I have spent more than five decades serving our country - in uniform and out - and of all the exceptional men and women I have worked with over the years, I can honestly say that Dave Petraeus stands out as one of our nation's great patriots."
CIA deputy director Michael Morell will serve as acting director of the agency, the White House confirmed. Eventually Mr Obama must nominate a new director to head the agency, who will then need to be confirmed by the Senate.
Mr Morell, who is well respected at both the White House and on Capitol Hill, also served as acting director following the departure of former CIA chief Leon Panetta.
The CIA faces a potential period of instability after Mr Petraeus' resignation, as it also deals with a budget plateau and questions over its response to a deadly attack at a US consulate in Benghazi, Libya.
SOURCE BBC

November 7, 2012

Wazee Kiteto wanufaishwa na Mfuko wa Maendeleo TASAF

Mwandishi Mary Mwita ,akimhoji Bibi Kizee ,aliyesaidiwa mbuzi na TASAF ,Wilaya ya Kiteto ,adai mbuzi wamemuungezea maisha kwa kuwa anapata maziwa na kupata lishe bora






















Kijana wa miaka 28 amkaba Mkurugenzi  AICC uchaguzi  wa NEC  Meru

VIJANA wameonekana kungara katika nafasi mbali mbali za uongozi wa Chama cha Mapinduzi  hususani katika nafasi ya NEC ambayo awali ilionekana kuwaniwa  na wakongwe wa siasa huku vijana wakipewa kisogo.

Katika Wilaya Meru ,Kijana  Julius Mungure,( 28 )alishangaza umati wa wanachama wa CCM  na wapenzi wa  CCM waliokuwa katika Hotel ya Ngurudoto  ,pale alivyosimama kujinadi na kuomba kura kwa kumwaga sera za mapinduzi ya maendeleo  na kumuangusha kinara na mkongwe katika Chama hicho   

 Mungure  mwenye umri wa  (28) ameshinda kwa kishindo  nafasi ya Halmashauri kuu ya Taifa  CCM (NEC )   kupata kura 575  dhidi ya mpinzani wake katika nafasi hiyo Elishilia  Kaaya ambaye ni Mkurugenzi wa AICC Mjini Arusha .

Ni wazi kuwa hakuna mtu aliyetarajia matokeo hayo kwa kuzingatia ukweli kuwa mchuano ulikuwa mkali  na Kijana huyo alionekana ana umri mdogo ,na wengi hakujua kama anauwezo wa kusimama na kujinadi katika jukwaa

Wapenzi wa Chama hicho walihudhuria katika uchaguzi wa nafasi mbali mbali ikiwa ni pamoja na NEC wamejigamba  kuwa wanahitaji damu changa ya vijana ili waweze kupata fikira mpya za  maendeleo katika chama

Joel Kaaya mwanachama wa CCM alisema kuwa wakati umefika wa Vijana kupewa nafasi kuongoza ikiwa ni kuwandaa kuwa viongozi bora hapo baadaye ,baada ya wazee kuachia madaraka .

Kwa upande wake Julius Mungure anasema  kuwa anatarajia kuwa kwa ushirikiano na wanachama  na wapenzi wa CCM watapiga hatua ya maendeleo ,na kueleza  anajipanga kuungana na vijana wenzake kuleta umoja katika chama na kuvunja makundi.

“Naamini kuwa umoja ni nguvu ,utengano ni udhaifu ,nikiwa kijana natarajia kuhamasisha mshikamano kwa vijana wenzangu bila kubagua ,ikiwa ni harakati  za kujipanga kuunda vikundi vya maendeleo ,na kuepuka kukaa vijiweni .”anasema Mungure

Anasema kuwa Vijana wa sasa ndiyo wanatarajiwa kujenga na kuimarisha amani katika nchi ,kuwa ni vyema wakaandaliwa mazingira bora ya kiuchumi  mapema ,ikiwa ni kuepusha ushawishi wa kujiingiza katika ushawishi wa kuingia katika Siasa chafu na kuwa vibaraka wa wanasiasa.

“Mimi kwa mtizamo wangu,naona kuwa tukiungana na kuwa na Sauti ya pamoja katika Chama chetu ni  wazi kuwa Vijana wengi watavutiwa na Chama na kuacha kutangatanga kuhamia katika vyama vingine.”anasisitiza Mungure.


‘Najivuna kuwa Kijana tena Mtanzania ndani ya Chama cha Mapinduzi ,na nikiri kuwa wapo wanasiasa walionifanya chama cha Mapinduzi ,wa kwanza ni Marehemu  Jeremia Sumari ,ambaye siasa zake zilikuwa za kistaarabu  na aliongoza kwa hekima ,na ndiyo maana akaweza kuongoza kwa vipindi viwili .”anasema Mungure.

Mwingine ni  Justin Salakana ,ambaye ni Mjomba wangu , na wengine wengi ,kwa kweli natamani kushirikiana na wenzangu ,ili kwa pamoja tuondoe makundi ambayo hayana msingi wowote wa maendeleo ,lakini kuharibu Chama kwa kweli ,kuna haja yakubalika na kuwa kitu kimoja katika Chama” anasema  Mungure

Hata hivyo anaema kuwa  baadhi ya vijana wamekata tamaa kutokana na hali maisha ,na kueleza  kuwa akiwa mchumi anatajipanga na wenzake jinsi ya kuanzisha miradi ya maendeleo ,hatimaye kuwawezesha vijana wenzake kujiajiri  na kuepuka kuwa tegemezi katika jamii wanazoishi.

Mungure ni msomi  mwenye Shahada mbili  za masuala ya Uc humi na Uwekezaji ,na kwa sasa anafanya kazi katika  kampuni ya Experience  Tanzania .




November 6, 2012

Yatima Mkoa wa Arusha wapatiwa msaada na Mbunge C HADEMA

Mbunge wa Vitim Maalum CHADEMA Mkoa wa Arusha ,Joyce Mukya akitoa msaada kwa baadhi ya watoto Yatima Mkoa wa Arusha 

Mbunge CHADEMA apania kusaidia Yatima Arusha


Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Joyce Mkukya akizungumza  na waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha ,kuhusu nia yake ya kusaidia watoto Yatima wa vituo mbali mbali Mkoa wa Arusha 

Madiwani wa Tarime wakunwa na Maendeleo ya Halmashauri ya Arusha

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha ,Halifa Hida akielezea mafanikio ya Halmashauri hiyo kwa timu ya  Madiwani kutoka Tarime ,walipozuru Halmashauri hiyoAdd

November 5, 2012

Kikwete afurahishwa na Huduma ya Afya Hospitali ya Oltrument,Arumeru

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Arusha Dk.Thobias Mkina akitoa ufafanuzi wa Hospitali ya Oltrument kwa Rais KikweteAdd caption

RAIS PIA ALIWATEMBELEA WAGONJWA WALIOLAZWA NA KUWAPA POLE

Rais Kikwete akisalimiana na mmoja wa wa wagonjwa aliyelazwa katiks hospitali ya Olturumet muda mfupi kabla ya kuizindua

ZIARA WILAYANI SIMAJIRO

Mwandishi Mary Mwita akifanya mahojiano  na Bibi Mariam  mkazi wa Wilaya ya Simanjiro