August 3, 2013
July 31, 2013
Mwanamke Happiness akombolewa na wanawake wa SIAT
| Rais wa SIAT Anna Anatoli akielezea ,hali ya ukatili katika Wilaya ya Arumeru |
Ukatili wa Kijinsia Arumeru waota mizizi ,SIAT yavalia Njuga tatizo ,hilo ,Kalamu ya waandishi yanusuru baadhi ya wanawake
| Mwandishi Mary Mwita ,akiwa nje ya Mwanamke Happiness Soine aliyekumbana na Ukatili wa Kijinsia ,Kalamu ya Mary Mwita ,imesaidia mwanamke huyo kukombolewa na kujengewa nyumba na wasamaria wa SIAT |
Na Mary Mwita ,Arusha
Vitendo vya Ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanawake hapa
nchini kwa miaka ya hivi karibuni vimepungua kutokana na jitihada za wadau wa
kutetea haki za binadamu kuvalia njuga tatizo hilo ,kwa kuwachukulia hatua
wahusika .
Wanawake katika
baadhi ya jamii wameonekana hawana haki ,na hivyo kunyanyaswa na hata kunyanganywa mali walizochuma na wanaume zao ambao wametangulia
mbele ya haki .
Katika Wilaya ya Arumeru ,ukatili dhidi ya wanawake
,umejikita katika baadhi ya jamii,wanawake wakinyanyaswa na hata kufukuzwa katika nyumba walizojenga
na wanaume zao .
Mfano halisi ni wa mwanamke Happiness Soine aliwahi kuandikwa katika gazeti la
Mtanzania mwaka 2010 kuwa alikuwa ananyanyaswa na shemeji yake ,ambaye alidaiwa kumiga na
kumjeruhi katika sehemu nyeti .
Wadau wa maendeleo baada ya kusoma habari hiyo ,iliyokuwa
imeandikwa na Bi Mary Mwita ,walivyalia njuga tatizo hilo ,na kufanikiwa kufika
kijijini kwa Happiness katika Kata ya Kingori ,Wilaya ya Arumeru .
Umoja wa wanawake wanataaluma unaoujulikana kama SIAT(Soroptimist International
Arusha Tanzania) ,yenye Makao
Makuu Mkoa wa Arusha ndiyo walioguswa na
mkasa wa Happiness na kulazimika kuwachukulia hatua wahusika na mwanamke huyo
kuwa huru .
Wanawake hao wakiongozwa na Rais wa Umoja huo ,Anna Anatoli walifanikiwa kushughulikia kesi feki zilizokuwa
zimefunguliwa kumkadamiza Bi Happiness,kuwafikisha
mahakamani watuhumiwa na kumjengea
nyumba ambayo imezinduliwa na Katibu Tarafa
katika Halmashauri ya Meru ,Bwana Sumari aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Arumeru .
Rais Anatoli akitoa simulizi ya mkasa wa Happiness anasema
kuwa ipo haja ya wadau wa haki za binadamu kuendelea kusaidia jamii husani wanawake wanaokadamizwa
na kunyimwa haki katika jamii wanazoishi .
Anapongeza waandishi wa habari kwa kutumia kalamu zao vyema
kumwulika maovu na kuyaanika katika jamii ,na kueleza kuwa kama isingekuwa ni
kalamu ya Mary Mwita wasingeweza kujua taabu na mateso aliyokuwa anapata
mwanamke huyo .
Anafafanua kuwa umoja na Shirika lao ,nilakujitolea ,hawana
wafadhili ,wanajitolea kujichangisha kama wanawake wanataaluma mbali mbali
,ikiwa lengo lao ni kuona kuwa wanawake wenzao wanaishi kwa amani na furaha na kusaidia familia zao
Ana Anatoli anasema
kuwa pia wameweza kusaidia wasichana zaidi ya 100 waliokuwa wanajihusisha na
vitendo vya ngono kabla ya wakati na kuwa waliobainika kuathirika na vitendo
hivyo wanaendelea kuangaliwa kwa ukaribu ,ikiwa ni kuwawezesha kurudi na kuishi
maisha ya kawaida na kujishughulisha kiuchumi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Munasa Nyerembe
katika taarifa yake iliyosomwa na Katibu Tarafa Bw,Sumari anasema kuwa
,Serikali kwa kushirikiana na wadau wa
Haki za Binadamu itaendelea itaendelea kuhakikisha kuwa makundi yote katika
jamii yanaishi kwa amani na kutendewa haki
na kuwaajibisha wanaowanyanyasa .
Nyerembe anapongeza wanawake hao na kuwataka kuendelea
kusaidia makundi zaidi katika jamii ,na kueleza kuwa Serikali inatambua mchango
wa wao na kuwa Serikali haiwezi kutekeleza majukumu pekee yao bila kupata msaada kutoka kwa wadau
wa maendeleo kama SIAT
Mkuu huyo pia anachukua fursa hiyo kupongeza jitihada za
Mwandishi Mary Mwita zakuandika habari za kweli ,na kuwezesha wahusika kuchukua
hatua stahiki kama alivyofanikisha habari ya Mwanamke Happiness kufikia umma wa
Watanzania na kujitokeza kumsaidia na kumjengea Nyumba .
Aidha anasema Serikali haitawaonea haya watu wanaonyanyasa wanawake na kueleza kuwa
Serikali itaendelea kufuatilia tatizo la Happiness ,ikiwa ni kuhakikisha kuwa anaishi
kwa amani ,na kukomesha ukatili dhidi yake na mashemeji zake ,ambao wanataka
kumyanganya mali alizochuma na mume wake.
Halmashauri ya Meru ,ni miongoni mwa Halmashauri hapa nchini
ambazo ukatili dhidi ya wanawake umejikita ,ni jukumu la wadau kuvalia njuga
tatizo hilo.
July 17, 2013
Nane Nane Kanda ya Kaskazini kufana mwaka huu
| Mwenyekiti wa TASO Kanda ya Kaskazini Athur Kitonga ,wakati wa mahojiano na blog hii |
Maonesho Nane Nane Kanda ya Kaskazini kutoa tafsiri ya Mapinduzi ya Kilimo na Mifugo,Washiri 324 kutoka ndani na
nje wadhibitisha kushiriki
Na Mary Mwita, Arusha
MAONESHO ya Nane nane(TASO) yanafungua milango kwa wadau wa kilimo na
mifugo kubadilishana uzoefu wa shughuli zao na hatimaye kuzalisha kwa
ubora mazao yanayotokana na mifugo na
kilimo.
Maonesho hayo hufanyika kila
mwaka ikiwa walengwa wakuu ni wakulima
na wafugaji ,ambao wanapata fursa yakuonyesha bidhaa zao za mifugo
Kauli mbiu ya maonesho hayo
mwaka huu ni Zalisha mazao ya kilimo na
mifugo kwa kulenga mahitaji ya soko .
Katika kanda ya Kaskazini
inayohusisha mikoa ya Arusha ,Manyara na Kilimanjaro maandalizi yamekamilika kwa
zaidi ya asilimia 75 .
Mwenyekiti wa TASO Kanda ya Kaskazini, Athur Kitonga anasema
kuwa wadau wa maonyesho tayari wameandaa maeneo yao ya maonesho ikiwa ni pamoja
na kupanda vipando vya mazao mbali mbali katika maeneo husika
Kitonga anabainisha kuwa
maonesho ya mwaka huu yanatarajiwa kuvunja rekodi kwa kuwa tayari washiriki wa
maonesho 324 wamedhibitisha kushiriki
,ikiwa ni kutoka ndani na nje ya nchi
Anataja baadhi ya washiriki
kuwa ni kutoka nchi ya Kenya ,Rwanda ,Burundi
na Pakistani .
Washiriki wa ndani ni Taasisi
za Serikali ,watu binafsi ,makampuni ya bidhaa za kilimo na mifugo na wadau
wengine wa maendeleo ya kilimo na mifugo .
Halmashauri za Wilaya zikiwa
ni wadau muhimu katika maonesho hayo ,wanatarajiwa kuandaa wakulima na wafugaji
kushiriki katika maonesho hayo ,kwa kuwagharamia usafiri na malazi.
Kitonga anasema kuwa katika
kuwezesha wakulima na wafugaji kujifunza mbinu bora za kilimo na mifugo mwaka
huu ,wameomba kila Halmashauri ilete wakulima na wafugaji 100.
Anasema kuwa washindi bora
watazawadiwa na TASO kwa kushirikiana na Halmashauri zao .
Pamoja na mambo mengine
anasema kuwa wamedhamiria kuhamasisha ufugaji bora ,kuwa wafugaji watazawadiwa
wakilenga wilaya mahiri kwa ufugaji wa mifugo ,ikiwa ni kuamusha ari ya kufuga
mifugo kwa ubora kwa kufuata mfumo bora
wa ufugaji.
Katika kuboresha mazingira
,anasema kuwa tayari wameweza kupanda miti 1000,ikiwa ni kuwezesha kuboresha
mazingira kwa ajili ya kizazi kilichopo na kijacho
Kitonga anawaondowa wasiwasi
wananchi watakaoshiriki katika maonesho hayo kuwa Usalama uko wa kutosha na
kuwa kampuni ya Intellegence Securio kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa
wa Arusha wamejizatiti kuhakikisha kuwa ulinzi unakuwa imara ,na kuwa hakuna
haja yakuwa na hofu yakutembelea na
kushiriki katika maonesho ya Nane Nane Mkoa wa Arusha .
Anasema kuwa Maonesho hayo
yatafunguliwa na Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini Magessa Mlongo na kufungwa na
Makamu wa Rais Mohamed Bilali
Akizungumzia maendeleo ya
Uwanja huo Kitonga anasema kuwa uwanja huo ,unatarajiwa kuleta maendeleo
makubwa ya kilimo na mifugo ,kwa kuwa wanatarajia kujenga Hosteli kwa ajili ya
wadau wa maonesho itakayowezesha kulala na kujifunza mbinu za kilimo na mifugo
.
Kitonga anavunja ukimya kwa
kueleza kuwa ujenzi wa Hosteli huo
unatarajiwa kuchangiwa na Serikali ikiwa watatoa Tshs million 300 ,ahadi
iliyotolewa na Profesa Jumanne Maghembe wakati wa Sherehe za Nane Nane mwaka
2011 Mkoa wa Arusha .
Pia anasema kuwa wanatarajia
kujenga Chuo bora cha mifugo na kilimo katika Uwanja wa Nane Nane ,Njiro Mkoa
wa Arusha ,ambacho kitatoa elimu ya kilimo na mifugo ,na kuwezesha wahitimu
kutumia elimu yao kusaidia jamii kufuga na kulima kwa ubora zaidi .
“Chuo hicho usajili wake uko
katika hatua za mwisho ,na kwa kweli Chuo hicho kitafungua mlango kwa watu
kujifunza kilimo na mifugo ,na hapa Nane nane ,itakuwa ni sehemu ya mafunzo kwa
vitendo ,lengo kuu ni kuona watu wanafanya shughuli zao kwa tija ,baada ya
kupatiwa elimu “anasema Kitonga
Kitonga anawahitimisha mahojiano na mwandishi wa
Makala hii kwa kuwakaribisha wananchi kushiriki katika maonesho hayo ikiwa na
kueleza kuwa maonesho ya mwaka huu yanatarajiwa kuvunja rekodi na kuwa miundo
mbinu ya uwanja imeimarishwa .
July 3, 2013
Wananchi Kiteto wasifu TASAF ,wataka wadau wengine kuiga mfano wa TASAF ,kwa kushirikisha wananchi kupanga na kusimamia wenyewe miradi husika
Mwandishi Mary Mwita ,akiwa Kiteto Manyara kihoji wananchi jinsi walivyonufaika na TASAF,wadai wamenufaika kwa kupata barabara ya uhakika walioichimba na kuitengeneza wenyewe ,wataka miradi mingine ya maendeleo ifuate nyayo za TASAF,kwa kuwa inashirikisha wananchi katika kila hatua ,na hivyo imeweza kufanikiwa kutokana na ushiriki wa wananchi ,na hivyo kuondoa mianya ya wanaofuja fedha za miradi
June 28, 2013
Mkurugenzi TAMIHA Crispin Mugarula akizungumza na Yatima anaowalea na kuwatunza
|
Mkurugenzi wa TAMIHA Crispin Mugarula ,akizungumza na watoto Yatima anaowalea na kuwasomesha ikiwa ni kati ya watoto 194 ,wanaosoma Shule ya St.Vivian Maji ya Chai ,Arumeru ,Arusha ,shule iliyoanzishwa na Mkurugenzi huyo kwa ajili ya watoto Yatima na watoto wengine wa jamii ya Meru na Mkoa wa Arusha
Arusha yajizatiti kutoa huduma ya Afya
Na Mary Mwita ,Arumeru
AFYA bora za watu katika jamii yeyote duniani
ni matokeo ya maendeleo kwa kutokana
na ukweli kuwa nguvu kazi za watu ni muhimu katika uzalishaji ambapo watu
wenye afya njema ,wanahitajika kushiriki katika shughuli husika .
Kutokana na uhalisia huo ,Halmashauri ya Arusha
katika Wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha kupitia wataalam wa Afya na watendaji
wa Halmashauri hiyo wanafanya kila jitihada kuhamasisha watu kujenga
utamaduni wa kupima Afya zao na kubaini matatizo yanayokabili kiafya na
kupata tiba mapema .
Wanawake
katika jamii hiyo wanapewa elimu kuhusu umuhimu wa kuhudhuria katik
vituo vya afya hususani wakati wa ujauzito ikiwa ni kuwalinda watoto wao toka
wakiwa tumboni ,kwa kupata ushauri wa kitaalam ,ikiwa ni pamoja na kuwakinga
watoto dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.
Miongoni wa wananchi waliopata elimu ya afya ya
uzazi na kuhimizwa kuchangia huduma ya afya ni wananchi wa Olkokola ,katika
Halmashauri ya Arusha ,elimu iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya
Arusha Dkt. Tobias Mkina
Mkina mtaalam wa Afya anawataka akina mama kujenga
utamaduni wa kuhudhuria Kliniki mapema ,kuepusha madhara wakati wa kujifungua
.
“Akina mama ,ninawaomba sana mjenge utamaduni kwa
kwenda kliniki ,kwa kuwa baadhi ya akina mama hapa ,bado wanajifungulia
nyumbani kwa msaada wa wawakunga wa jadi ,ninawaomba sana ,mjali afya zenu
,msipende kujifungulia nyumbani ,munaweza kupata madhara ikiwa ni
pamoja na kifo .”anasema Mkina
“Kwa sasa hakuna kisingizio cha ukosefu wa Hospitali
,maana kuna hii hospitali ya Oltrument iliyozinduliwa na Mheshimiwa Rais
Jakaya Kikwete ,hivyo ninawaomba sana ,muitumie vyema kwa ajili ya
kupata huduma bora za Afya .”anaongeza Mkina
Pamoja na mambo mengine anawataka wananchi wa jamii
hiyo ,kuchangia huduma ya mfuko
wa Afya jamii na kuwawezesha kupata huduma ya afya kwa mwaka
mzima ,ikiwa watalipa Tsh 10,000
Halmashauri hiyo ina jumla ya vituo vya kutolea
huduma za Afya 48 ,ikiwa ni Hospitali mbili ,moja ikiwa ni
Shirika la dini ambayo kwa sasa ni Hospitali Teule ya Halmashauri ya Arusha
Vituo vya afya ni 5 ,vya Serikali
vinne na kimoja kinamilikiwa na mtu binafsi ,Zahanati
41 ambazo kati ya hizo 25 ni za Seriali na 16 za Mashirika
na watu binafsi .
Huduma
za Afya zinazotolewa ni ,Huduma za wagonjwa wan je ,Huduma za Afya ya Kinywa
na meno ,Huduma ya Afya akili ,Huduma ya maabara na damu salama ,Huduma
za afya ya Uzazi na mtoto
Nyingine ni Huduma ya Ushauri
nasaha na Upimaji VVU ,Huduma za Utoaji wa dawa za
kupunguza makali ya Virusi vya Ukimwi ,Huduma za Kifua Kikuu na
Ukoma ,Huduma za Kifua Kikuu na ukoma ,Huduma za Kulaza Wagonjwa kwa baadhi
ya vituo
Akitoa ufafanuzi zaidi Dk.Mkina anasema kuwa wameipa
kipaumbele huduma ya Wazee ,kuwa katika Hospitali Teule ya Selian na
Hospitali ya Oltrument na kuwa
Robo ya mwaka Januari hadi March 2012 ,Wazee 121,wanawake wakiwa
58 na wanaume 63
Robo ya mwaka April hadi June 2012
,Wazee 226 wanaume 114, wanawake 112 na Robo ya mwaka Julai hadi
Septemba 2012 Wazee 301 wanawake wakiwa 110 na wanaume wakiwa 191
Mganga huyo anadai kuwa huduma ya afya kwa wazee
inaendelea kuboreshwa ilikuweza kunufaisha Wazee wengi zaidi .
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Arusha ,Fidelist Lumato anasema kuwa lengo la Halmashauri hiyo ni kuona
wananchi wa Halmashauri hiyo wakiwa wanapata huduma bora ya afya na
kuwawezesha kushiriki katika ujenzi wa Taifa .
Kimsingi anasema
kuwa majengo bora yamejengwa katika Hospitali ya Oltrument na ambayo kwa
kiasi kikubwa yameinua hadhi ya Hospitali hiyo ,na kuwa majengo hayo ni matanao na
yamegharimu Tshs 624,650,920.30
Anafafanua kuwa Jengo la Upasuaji
(Theatre) Tshs 118,339,526,Wodi ya Upasuaji (Surgical ward)
Tshs 140,878,004.10 ,Maabara Tshs 22,650,012.25 ,Wodi ya wanaume
134,365,871.35,Wodi ya Wanawake Tshs 154,751,002 .50,Ukarabati wa
Majengo ya Zamani Tshs 53,666,503
Lumato, anasema kuwa Jengo la Upasuaji limejengwa na
ufadhili wa Shirika la Umoja wa Madaktari wa Kijerumani la
Organization for International Medical Cooperation ( VIMZ).
Jengo la Wodi ya upasuaji limejengwa kwa ufadhili wa
Umoja wa madaktari wa Kijerumani na Halmashauri ya Arusha ikiwa
ni Tshs.55,728,004 na Tshs 85,150,000
Lumato anasema Jengo la maabara limejengwa kwa
msaada wa wafadhili wa kutoka Marekani kupitia Shirika la Centre for Disease
Control(CDC) pamoja na mashine za kisasa za uchunguzi wa magonjwa mbali mbali
Anaendelea kubainisha kuwa Jengo la Wodi ya wanaume
limejengwa kwa ushirikiano wa wananchi ,Halmashauri ya Wilaya ya Arusha chini
ya mpango wa mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF ) na kutokana na
mapato yake ya ndani Tshs 48,780,586 na Tshs 85,585,285.35
Mkurugenzi anasema Jengo la Wanawake limejengwa
mahususi kwa ajili ya kuwalaza akina mama na limejengwa mahususi
kwa ajili ya kuwalaza akina mama na limejengwa kwa kutumia ruzuku
ya serikali kupitia Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM),na
mchango wa Halmashauri kutokana na mapato ya ndani .
Pamoja na mambo mengine anasema kuwa Hospitali
hiyo inakabiliwa na matatizo mbali mbali ikiwa ni ukosefu wa majengo
muhimu yatakayokidhi mahitaji ya ongezeko la wagonjwa wa nje na kulazwa
Anataja majengo hayo kuwa ni Jengo la Wagonjwa wa
nje na Utawala (OPD),Wodi ya watoto ,Jengo la kituo cha uangalizi na
kutolea huduma kwa waathirika wa virusi vya Ukimwi,tiba na ushauri
nasaha, Jengo la X ray pamoja na mashine ya X Ray na Jengo la kusubiria
kujifungulia .
Kimsingi anasema kuwa Hospitali hiyo
inatarajiwa kupunguza vifo vya watoto na wajawazito ,na kuhimiza jamii
kujenga utamaduni wa kwenda katika vituo vya afya kupima afya zao ,na kuepuka
kusubiri hadi mgonjwa kuzidiwa na kuwa na hali mbaya ndipo anapelekwa
hospitali
Lumato anahimiza wananchi wa Halmashauri hiyo
kujiunga na mfuko wa huduma ya Afya na kuchangia Tshs 10,000 ambazo mwananchi
ataweza kutibiwa kwa kipindi cha mwaka mmoja pamoja na familia yake.
|
T
|
People (3)
Show details
|
Subscribe to:
Posts (Atom)