ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Kilutheri Tanzania ,Alex Malasusa
amesema kuwa Chuo Kikuu Tumaini
kimelenga kuwaandaa viongozi na wasomi
bora watakaosaidia kuleta maendeleo ya nchi,na kuwa suala la maadili
linatiliwa mkazo .
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza
kuwatunuku vyeti wahitimu 470 wa shahada mbali mbali waliomaliza chuoni hapo
anasema kuwa maadili yanaendana na mavazi na kuwa zoezi la kuwashughulikia
wanafunzi wanaovyaa nguo zinazowadhalilisha linaendelea ,na kuwa Uongozi wa
vyuo hivyo umelivalia njuga .
Askofu Malasusa anasema kuwa inajukumu lakuunga mkono
jitihada za Chuo hicho kwa kuhakikisha kuwa wanaonya watoto wao kuacha kuvaa
mavazi ambayo siyo rasmi na kueleza kuwa jukumu la kuwalea watoto na wanafunzi
linatakiwa kuanzia katika jamii na familia .
No comments:
Post a Comment