November 21, 2012

Helikopta za Umoja wa Mataifa zashambulia wapiganaji Congo

Jeshi la MONUSCO laingia kati Goma

 
Mpiganaji wa M23 kaskazini ya Goma
Helikopta zenye silaha za Umoja wa Mataifa zimeshambulia maeneo ya wapiganaji mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, huku mapambano yanaendelea baina ya jeshi la Congo na kundi la wapiganaji wa M23.
Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kuweka amani, Monusco, kimesema kuwa vikosi vya jeshi la serikali kaskazini ya mji wa Goma, vilishambuliwa Jumamosi asubuhi, na kufanya raia kulikimbia eneo hilo na helikopta za Umoja wa Mataifa kutumwa huko.
Monusco ina idhini ya kuwalinda raia na kuwasaidia wanajeshi wa serikali ikihitajika.
Hakuna idadi iliyotolewa ya maafa yaliyotokea.
Umoja wa Mataifa unazilaumu Rwanda na Uganda kwamba zinawaunga mkono wapiganaji - tuhuma ambazo nchi hizo inakanusha.

No comments:

Post a Comment