Mripuko Nairobi wazusha fujo
Watu wanakadriwa watano wamekufa katika mripuko kwenye mtaa wa Eastleigh wa Nairobi wenye wakaazi wengi wa Kisomali.
Naibu msemaji wa polisi wa Kenya, Charles Owino, alieleza kuwa bomu liliripuka ndani ya basi lilipokuwa likipita mtaa wa Eastleigh.
Dakika chache baadae vijana waliokuwa na hasira waliwalenga watu wa jamii ya Kisomali kwenye mtaa huo.
Mtu aliyeshuhudia tukio hilo aliiambia BBC kwamba aliona makundi ya Wasomali wakijipanga kupambana na vijana hao ambao walikuwa wakivamia nyumba zao.
Polisi ilibidi kufyatua risasi hewani kuwatawanya watu.
Hili ni shambulio la karibuni kabisa katika miji ya Kenya tangu jeshi la nchi hiyo kuingia Somalia mwaka jana.
No comments:
Post a Comment