Kutoka Mahakamani
Mahakama yatoa hukumu ya
Talaka yadai talaka inayodaiwa ni batili
,Siyo ya Mke wa Kisheria mgawanyo wa mali wagonga mwamba
Na Mwandishi wetu
MAHAKAMA ya Mwanzo Mbagala,
Dar es Salaam imesema haiwezi kumuamuru Mmiliki wa shule nne za Shule za Sekondari, St Mathew na St
Marks ,Thadei Mtembei kutoa talaka kwa Magreth Mwangu kutokana na ndoa yao kuwa
batili
Akisoma hukumu hiyo leo,
Hakimu Rajab Tamambele alisema ndoa aliyofunga Mwangu pamoja na Mtembei ambayo
ni ya kimila ni batili kwa kuwa mdai hakutoa cheti cha ndoa hiyo ilipofungwa
Alisema kwa misingi hiyo,
mahakama haiwezi kumuamuru Mtembei kutoa talaka kwani aliwasilisha cheti cha
ndoa ya mke mmoja aliyoifunga mwaka 1985
mahakama hiyo haiwezi kugawa
mali kama ambavyo mdai ameiomba mahakama, ambapo amesisitiza kuwa mgawanyo wa
mali unatokana na ndoa halali ambayo baba na mama wanaishi pamoja.
‘’Mashahidi wote wameeleza
kuwa Mtembei na Mwangu walikuwa wanakutana hoteli ya Sleep Inn. Kwa hivyo
mahakama inaona kuwa uhusiano kati ya mdai na mdaiwa ulikuwa wa kimapenzi pekee
au hawara na kwa lugha ya kistaarabu tunaita mzazi mwenzie,’’ aliongeza
Tamambele.
Alifafanua kuwa kulipa mahari ambapo mdai
aliieleza mahakama kuwa alitolewa ng’ombe watano, sio njia ya kufunga ndoa bali
ni kuelekea kufunga ndoa.
Aliendelea kusema kuwa
kitendo cha baba kupewa mahari akiwa peke yake bila ya kuwa na mzee wa kabila
hilo kuthibitisha, sio sahihi katika sheria za ndoa.
Akisoma hukumu hiyo kwa saa
moja, Hakimu Tamambele alisema kuwa watoto watatu kati ya Mtembei na Mwangu wamezaliwa
nje ya ndoa, hivyo mahakama haiwezi kuamuru watoto hao kupatiwa matunzo.
‘’Mdaiwa anatakiwa kushukuru
kitendo cha mdai kujenga nyumba tatu kwa ajili ya watoto kwani wengine hawawezi
kufanya kitu kama hicho. Kila mzazi anatakiwa kuwatunza watoto hao, ’’ alisema.
Akizungumzia kuwakilishwa
kwa mdaiwa, alisema kwa mujibu wa sheria ya kama mdaiwa ni mgonjwa anaweza
akawakilishwa ambapo mtoto wake, Peter ndiye alichukua nafasi ya kumuwakilisha
baba yake.
Aidha, alisema haki ya
kukata rufaa kwa mdai iko wazi na kwamba inatakiwa kukatwa kwa siku 45.
Katika kesi hiyo ambayo
ilifunguliwa Juni 5, mwaka huu, Mwangu aliiomba mahakama kumuamuru mdaiwa kutoa
talaka, matunzo ya watoto na ya machumo ya pamoja yenye thamani ya Sh milioni
800.
Alisema kesi hiyo ilikuwa na
jumla ya mashahidi nane ambapo watano kutoka upande wa mdai na watatu
upande wa mdaiwa.
Mdai katika kesi hiyo alifungua kesi kupitia ofisi ya Ustawi wa jamii na ilipoanza kusikilizwa mdai alisema walianza mahusiano mwaka 1995 ambapo walizaa watoto watatu na walijenga shule nne, nyumba pamoja na hoteli tatu za Dar es Salaam na Bukoba |
CCM HATUHITAJI AHADI, TUNAHITAJI MTU MWENYE KUPAMBANIA WANANCHI WAKE - NDG.
ISSA GAVU
-
> CCM Yakemea viongozi wenye kujihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na
kukandamiza watu.
" Kwa mujibu wa ibara ya 16 inamtaja nani kiongozi, maana yake...
7 hours ago
No comments:
Post a Comment