Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Phillipo
Mulugo, Mulugo alisema baada ya wizara yake kupata taarifa za mgogoro
imechukua hatua ya kumwagiza Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Bagamoto
kupeleka taarifa za chanzo ili hatua zichukuliwe haraka.
Jumatatu wiki hii Mkuu wa Mkoa wa Pwani,
Mwantumu Mahiza, alitangaza kuifunga shule hiyo kwa kipindi
kisichojulikana kutokana na mgogoro wa kidini katika shule hiyo ambao
upelekea amani kutoweka.
Mahiza alisema amechukua uamuzi huo ili
kuiwezesha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Wizara ya Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kutafuta ufumbuzi wa migogoro,
utoro wa walimu na kudumisha amani katika shule hiyo.
“Baada ya kufika nimebaini bado kuna
tatizo, kwani hadi nafika jana (juzi) nimekuta wanafunzi 356 kati ya 740
walioandikishwa katika shule hiyo hawajulikani walipo na Mkuu wa Shule
hajui walipo,” alisema Mahiza.
Hata hivyo, taarifa ambazo NIPASHE
ilizipata toka shule hapo zinaeleza kuwa kufungwa kwa shule hiyo
kulifuatia wanafunzi tisa kuandikiwa barua ya kusimamishwa masomo,
maamuzi ambayo yaliamriwa na Bodi ya Shule hiyo, lakini wanafunzi hao
walikataa kuzipokea barua hizo.
Baada ya wanafunzi hao kukataa kuzipokea
barua hizo, kulizuka vurugu za wanafunzi shule hapo ambao walikuwa
wakiwaunga mkono wanafunzi walioandikiwa barua hizo na hivyo serikali ya
mkoa kuchukua hatua ya kuifunga shule kwa muda usiojulikana.
No comments:
Post a Comment