November 7, 2012

Wazee Kiteto wanufaishwa na Mfuko wa Maendeleo TASAF

Mwandishi Mary Mwita ,akimhoji Bibi Kizee ,aliyesaidiwa mbuzi na TASAF ,Wilaya ya Kiteto ,adai mbuzi wamemuungezea maisha kwa kuwa anapata maziwa na kupata lishe bora






















Kijana wa miaka 28 amkaba Mkurugenzi  AICC uchaguzi  wa NEC  Meru

VIJANA wameonekana kungara katika nafasi mbali mbali za uongozi wa Chama cha Mapinduzi  hususani katika nafasi ya NEC ambayo awali ilionekana kuwaniwa  na wakongwe wa siasa huku vijana wakipewa kisogo.

Katika Wilaya Meru ,Kijana  Julius Mungure,( 28 )alishangaza umati wa wanachama wa CCM  na wapenzi wa  CCM waliokuwa katika Hotel ya Ngurudoto  ,pale alivyosimama kujinadi na kuomba kura kwa kumwaga sera za mapinduzi ya maendeleo  na kumuangusha kinara na mkongwe katika Chama hicho   

 Mungure  mwenye umri wa  (28) ameshinda kwa kishindo  nafasi ya Halmashauri kuu ya Taifa  CCM (NEC )   kupata kura 575  dhidi ya mpinzani wake katika nafasi hiyo Elishilia  Kaaya ambaye ni Mkurugenzi wa AICC Mjini Arusha .

Ni wazi kuwa hakuna mtu aliyetarajia matokeo hayo kwa kuzingatia ukweli kuwa mchuano ulikuwa mkali  na Kijana huyo alionekana ana umri mdogo ,na wengi hakujua kama anauwezo wa kusimama na kujinadi katika jukwaa

Wapenzi wa Chama hicho walihudhuria katika uchaguzi wa nafasi mbali mbali ikiwa ni pamoja na NEC wamejigamba  kuwa wanahitaji damu changa ya vijana ili waweze kupata fikira mpya za  maendeleo katika chama

Joel Kaaya mwanachama wa CCM alisema kuwa wakati umefika wa Vijana kupewa nafasi kuongoza ikiwa ni kuwandaa kuwa viongozi bora hapo baadaye ,baada ya wazee kuachia madaraka .

Kwa upande wake Julius Mungure anasema  kuwa anatarajia kuwa kwa ushirikiano na wanachama  na wapenzi wa CCM watapiga hatua ya maendeleo ,na kueleza  anajipanga kuungana na vijana wenzake kuleta umoja katika chama na kuvunja makundi.

“Naamini kuwa umoja ni nguvu ,utengano ni udhaifu ,nikiwa kijana natarajia kuhamasisha mshikamano kwa vijana wenzangu bila kubagua ,ikiwa ni harakati  za kujipanga kuunda vikundi vya maendeleo ,na kuepuka kukaa vijiweni .”anasema Mungure

Anasema kuwa Vijana wa sasa ndiyo wanatarajiwa kujenga na kuimarisha amani katika nchi ,kuwa ni vyema wakaandaliwa mazingira bora ya kiuchumi  mapema ,ikiwa ni kuepusha ushawishi wa kujiingiza katika ushawishi wa kuingia katika Siasa chafu na kuwa vibaraka wa wanasiasa.

“Mimi kwa mtizamo wangu,naona kuwa tukiungana na kuwa na Sauti ya pamoja katika Chama chetu ni  wazi kuwa Vijana wengi watavutiwa na Chama na kuacha kutangatanga kuhamia katika vyama vingine.”anasisitiza Mungure.


‘Najivuna kuwa Kijana tena Mtanzania ndani ya Chama cha Mapinduzi ,na nikiri kuwa wapo wanasiasa walionifanya chama cha Mapinduzi ,wa kwanza ni Marehemu  Jeremia Sumari ,ambaye siasa zake zilikuwa za kistaarabu  na aliongoza kwa hekima ,na ndiyo maana akaweza kuongoza kwa vipindi viwili .”anasema Mungure.

Mwingine ni  Justin Salakana ,ambaye ni Mjomba wangu , na wengine wengi ,kwa kweli natamani kushirikiana na wenzangu ,ili kwa pamoja tuondoe makundi ambayo hayana msingi wowote wa maendeleo ,lakini kuharibu Chama kwa kweli ,kuna haja yakubalika na kuwa kitu kimoja katika Chama” anasema  Mungure

Hata hivyo anaema kuwa  baadhi ya vijana wamekata tamaa kutokana na hali maisha ,na kueleza  kuwa akiwa mchumi anatajipanga na wenzake jinsi ya kuanzisha miradi ya maendeleo ,hatimaye kuwawezesha vijana wenzake kujiajiri  na kuepuka kuwa tegemezi katika jamii wanazoishi.

Mungure ni msomi  mwenye Shahada mbili  za masuala ya Uc humi na Uwekezaji ,na kwa sasa anafanya kazi katika  kampuni ya Experience  Tanzania .




No comments:

Post a Comment