Chuo Cha Maendeleo ya
Jamii ,kilichopika wasomi wanaotumikia Taifa ,lakini kiwa kinarembwa na majengo
Chakavu
NI jambo la kushangaza kushuhudia vyuo bora na muhimu hapa nchini
,vilivyopika wasomi ambao wapo wanatumikia Taifa ,vikiwa vimepewa kisogo na Serikali
,vikiwa vinarembwa na majengo chakavu , ambao yanaondoa yanashushia chuo
husika Sifa .
Wakati umefika wa Wadau wa maendeleo kushirikiana kuboresha
vyuo hivyo kwa kutambua wazi kuwa vyuo hivyo ni kwa ajili ya kizazi kilichopo
na kijacho ,kwa kuwa watoto na vijana wa kizazi kilichopo wanatarajiwa kujiunga
na kusoma katika vyuo hivyo .
Serikali haina budi kuacha mkono wa Birika ,kiasi cha kutenga bajeti kiduchu
kwa ajili ya kuendesha vyuo husika,vyuo
vya Serikali vinapaswa kuboreshwa na kuwa na muonekano kama ilivyo vyuo vya
watu binafsi hapa nchini ,kwa kuwa kila mtu anaamini kuwa Serikali ni bora
kuliko watu taasisi binafsi
Nalazimika kuandika makala hii baada yakuzuru baadhi ya vyuo
vya Serikali Mkoa wa Arusha na kukerwa na miundo mbinu mibovu ambayo ni majengo yaliyochoka na yalijengwa
wakati wa mkoloni,.
Serikali inapaswa kuona haya ,na kutenga fedha za kutosha mazingira bora ya wanataaluma
wanakwenda kusoma katika vyuo hivyo ,ikiwa ni hatua ya kuwawezesha kusoma
katika mazingira bora yanayovutia na hivyo kuweza kufaulu katika masomo
yao,hatimaye kumaliza na kutumikia Taifa lao.
Mpenzi msomaji miongoni mwa vyuo nilivyodhuru kuona uhalisia
wa miundo mbinu ni Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Tengeru kilichoanzishwa mnamo mwaka 1963 kikifundisha kozi ya Maendeleo ya Jamii kwa ngazi ya cheti.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo hicho Anatory Bunduki ,Mnamo mwaka
1983 Chuo kilianza kufundisha na
kutoa stashahada ya juu ya Maendeleo ya Jamii (Advanced Diploma) ikiwa na jumla
ya wanachuo 35 na wakufunzi 15 waanzilishi.
Bunduki anasema kuwa mwaka 2003 Chuo kilipata Ithibati rasmi kutoka kwa Baraza la Taifa la
Ufundi (NACTE) na kuanza kutoa stashahada ya juu katika kozi mbili zingine na
kufanya kozi kuwa tatu kama ambazo ni ;Usimamizi wa Program za Maendeleo ya Jamii(Management
of Community Development programmes),Jinsia na Maendeleo (Gender and
Development).
Nyingine ni Upangaji na uendeshaji shirikishi wa
Miradi(Project Planning and Managament).
Bunduki anafafanua kuwa mwaka 2008 Chuo hicho kilisitisha rasmi kudahili wanachuo katika
ngazi ya stashahada ya juu na kuanza kutoa mafunzo katika kozi zote tatu katika
ngazi ya shahada ya kwanza (Bachelors degree) na mwaka 2010/2011 Chuo
kilisitisha rasmi kutoa mafunzo katika ngazi ya stashahada ya juu (phasing out)
na kubaki na ngazi ya shahadaya kwanza.
Tangu kuanzishwa kwake Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Tengeru
Kiliwahi kuongozwa na wakuu wa Chuo wapatao nane( 8)kati ya hao wanawake wawili
Bi. Florence Ghamunga 1985-1986 na Bi.Celina Shinyambala 1994-1998.
Mkuu wa Chuo wa kwanza aliitwa Captain E.P.Machumu na Mkuu wa
Chuo wa sasa ni Bw. Anatory B.Bunduki.
Pamoja na changamoto Lukuki katika chuo hicho ,Bundi anasema
kuwa wameweza kutoa wahitimu 2,332 katika
fani zote tatu za Maendeleo ya Jamii tangu kilipoanzishwa wengi wao sasa wako
kazini.
Chuo kimeweza kupanda ngazi
tofauti katika utoaji wa mafunzo ambazo ni; ngazi ya Cheti, Stashahada ya juu, Shahada ya kwanza na Stashahada ya Uzamili.
Anaendelea kutoa historia ya chuo kuwa Chuo kinajumla ya wanachuo 543 ikiwa wanawake ni 308 na wanaume 235.Kwa upande wa wahadhiri anasema kina jumla ya wahadhiri 27, uwiano wa mhadhiri 1 kwa
wanafunzi 20.
Aidha anasema Chuo
kimeweza kujitangaza kwa njia mbalimbali, kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wadau mbali
mbali na kuhuisha michezo.
Katika kukabiliana na uhaba wa maji
Chuo hicho kimefanikiwa kujenga
kisima kirefu cha maji safi na salama kwa jumuiya ya Chuo cha Maendeleo ya
Jamii – Tengeru tangu 2003,
Hata hivyo anasema katika kuboresha miundo mbinu ya Chuo wameweza kujenga kumbi pacha mbili za mihadhara
zilizokamilika 2008, na kugharimu shs. 668,502,611.77/=
zikiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 600 kwa wakati moja.
Bunduki anasema kuwa wanaendelea na ujenzi wa maktaba ya kisasa unaotegemewa
kugharimu jumla ya shs.513,382,914/=
kwa awamu ya kwanza maktaba hii ikikamilika itakuwa na uwezo wa kuhudumia
wanafunzi 200 kwa wakati moja.
Kumekuwepo na tatizo la ukosefu wa fedha hivyo kuchelewesha awamu ya
pili ya ujenzi
Bunduki anasema kuwa wanakabiliwa na Changamoto Lukuki baadhi ya
changamoto hizo zikiwa ni Uchakavu wa miundo mbinu ikiwa ni madarasa, mabweni, nyumba za watumishi na
jengo la utawala,na kueleza kuwa uongozi
wa Chuo unajitahidi kufanya ukarabati wa
hatua kwa hatua hususani mabweni,
zahanati, madarasa na nyumba za watumishi ikiwa ni wakati fedha
zinapatikana .
Anavunja ukimya na kueleza kuwa
pamoja na kujitahidi kutoa huduma wanapata vikwazo na kufanya shughuli za chuo
kusuasua ,kuwa mahitaji ya uendeshaji wa Chuo mfano mwaka 2012/2013 ni Tshs. 5,147,758,984/-lakini fedha zinazopatikana kutokana na mapato ya ndani ni Tshs.
691,505,600/= ruzuku ni Tshs 49,583,000/=,
mishahara ni Tshs. 1,121,215,924/= sawa na asilimia 36.2 tu ya mahitaji halisi ya Chuo.
Bunduki anasema kuwa Chuo kinajitahidi kuainisha vyanzo vingine vya
mapato ikiwa ni pamoja na ada za mafunzo ya muda mfupi, utafiti na ushauri wa
kitaalamu.
Akizungumzia masuala mengine
anasema kuwa Chuo kinakabiliwa na uhaba wa vyombo vya usafiri hususani pale mafunzo ya vitendo
yanapohitajika na hata katika utendaji
wa majukumu ya kila siku, na kuwa Chuo kinakabiliwa na upungufu wa watumishi wa kada
mbalimbali ikiwemo wahadhiri na watumishi waendeshaji. Na kufanya huduma ya
taaluma kudorora .
Kwa upande wao baadhi ya watumishi wa Chuo hicho wameeleza
kuwa ,Maslahi duni yanawavunja moyo watumishi katika utendaji wao wa kazi wa kila siku, kwa
kuwa wanashindwa kumudu gharama za maisha zinazopanda kila wakati.
Watumishi hao wanasema kuwa
wanaweza kukabiliana na matatizo hayo
ikiwa Serikali itatoa fursa ya chuo kujiendesha na kujisimamia chenyewe
na mwongozo wa Utumishi kupitishwa.
Mkuu huyo anasema kuwa matarajio ya badae ni Chuo ni kitahuisha
mafunzo ya muda mfupi katika nyanja za uhamasishaji jamii, ubunifu na uandikaji
wa miradi, uandikaji taarifa, uongozi, haki za Mama na Mtoto, Ujasiriamali n.k.
Pamoja na kutoa mafunzo ya muda mrefu
chuo kinategemea pia kujikita katika ushauri wa kitaalamu na utafiti hususani
katika masuala ya kijamii.Chuo kwa kushirikana na bodi ya Uendeshaji na Wizara,
kimepata ithibati ya kujiendesha
kisheria katila utoaji wa mafunzo (AUTONOMY).
Kwa upande wao Afisa habari wa Chuo hicho Clara Emanuel
anasema kuwa Chuo kina mahusiano mazuri na vyuo vingine ,katika Nyanja ya
michezo na mijadala ya taaluma ,na kuwa kupitia michezo wanafunzi wameweza
kubadilishana uzoefu na kuepuka kujiingiza katika vitendo vya uhalifu
Anasema kuwa wanafunzi wengi katika Chuo hicho wamejikita
katika taaluma zao ,na kuwa muda mwingi wanatumia kujisomea ,na kueleza kuwa
nidhamu hiyo imetokana na uongozi bora wa chuo .
Kwa Upande wake mmoja wa watumishi katika maktaba ya Chuo cha
Maendeleo ya Jamii Tengeru Joseph Atanasi ,ambaye mwandishi wa makala
hii alifanya mahojiano nayo anasema kuwa vitabu havitoshelezi na kueleza kuwa
wanahitaji vitabu zaidi na bora vinavyoendana na wakati ,ikiwa ni kuwawezesha
wanafunzi kusoma kulingana na wakati ,
Anasema kuwa vitabu vilivyo ni vya miaka ya nyuma na kueleza
kuwa bado vinafaa kutumika lakini vitabu vipya vinahitajika kutokana nauhalisia
wa karne hii ya Sayansi na Tekenolojia .
Tangu kuanzishwa kwake Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Tengeru
Kiliwahi kuongozwa na wakuu wa Chuo wapatao nane( 8)kati ya hao wanawake wawili
Bi. Florence Ghamunga 1985-1986 na Bi.Celina Shinyambala 1994-1998.
Mkuu wa Chuo wa kwanza aliitwa Captain E.P.Machumu na Mkuu wa
Chuo wa sasa ni Bw. Anatory B.Bunduki.
Mwisho
No comments:
Post a Comment