May 5, 2013

Chuo cha Maendeleo jamii ,Kilichopewa kisogo na Serikali


Chuo Cha Maendeleo ya Jamii ,kilichopika wasomi wanaotumikia Taifa ,lakini kiwa kinarembwa na majengo Chakavu

NI jambo la kushangaza  kushuhudia vyuo bora na muhimu hapa nchini ,vilivyopika wasomi ambao wapo wanatumikia Taifa ,vikiwa vimepewa kisogo na Serikali ,vikiwa vinarembwa na majengo chakavu , ambao yanaondoa yanashushia chuo husika  Sifa .
Wakati umefika wa Wadau wa maendeleo kushirikiana kuboresha vyuo hivyo kwa kutambua wazi kuwa vyuo hivyo ni kwa ajili ya kizazi kilichopo na kijacho ,kwa kuwa watoto na vijana wa kizazi kilichopo wanatarajiwa kujiunga na kusoma katika vyuo hivyo .
Serikali haina budi kuacha mkono  wa Birika ,kiasi cha kutenga bajeti kiduchu kwa  ajili ya kuendesha vyuo husika,vyuo vya Serikali vinapaswa kuboreshwa na kuwa na muonekano kama ilivyo vyuo vya watu binafsi hapa nchini ,kwa kuwa kila mtu anaamini kuwa Serikali ni bora kuliko watu taasisi  binafsi
Nalazimika kuandika makala hii baada yakuzuru baadhi ya vyuo vya Serikali Mkoa wa Arusha na kukerwa na miundo mbinu mibovu  ambayo ni majengo yaliyochoka na yalijengwa wakati wa mkoloni,.
Serikali inapaswa kuona haya ,na kutenga fedha  za kutosha mazingira bora ya wanataaluma wanakwenda kusoma katika vyuo hivyo ,ikiwa ni hatua ya kuwawezesha kusoma katika mazingira bora yanayovutia na hivyo kuweza kufaulu katika masomo yao,hatimaye kumaliza na kutumikia Taifa lao.

Mpenzi msomaji miongoni mwa vyuo nilivyodhuru kuona uhalisia wa miundo mbinu ni Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Tengeru kilichoanzishwa  mnamo mwaka 1963 kikifundisha kozi ya Maendeleo ya Jamii kwa ngazi ya cheti.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo hicho Anatory Bunduki ,Mnamo mwaka 1983 Chuo kilianza kufundisha na kutoa stashahada ya juu ya Maendeleo ya Jamii (Advanced Diploma) ikiwa na jumla ya wanachuo 35 na wakufunzi 15 waanzilishi.
Bunduki anasema kuwa mwaka 2003 Chuo kilipata Ithibati rasmi kutoka kwa Baraza la Taifa la Ufundi (NACTE) na kuanza kutoa stashahada ya juu katika kozi mbili zingine na kufanya kozi kuwa tatu kama ambazo ni ;Usimamizi wa Program za Maendeleo ya Jamii(Management of Community Development programmes),Jinsia na Maendeleo (Gender and Development).
Nyingine ni Upangaji na uendeshaji shirikishi wa Miradi(Project Planning and Managament).
Bunduki anafafanua kuwa mwaka 2008 Chuo hicho  kilisitisha rasmi kudahili wanachuo katika ngazi ya stashahada ya juu na kuanza kutoa mafunzo katika kozi zote tatu katika ngazi ya shahada ya kwanza (Bachelors degree) na mwaka 2010/2011 Chuo kilisitisha rasmi kutoa mafunzo katika ngazi ya stashahada ya juu (phasing out) na kubaki na ngazi ya shahadaya kwanza.

Tangu kuanzishwa kwake Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Tengeru Kiliwahi kuongozwa na wakuu wa Chuo wapatao nane( 8)kati ya hao wanawake wawili Bi. Florence Ghamunga 1985-1986 na Bi.Celina Shinyambala 1994-1998.

Mkuu wa Chuo wa kwanza aliitwa Captain E.P.Machumu na Mkuu wa Chuo wa sasa ni Bw. Anatory B.Bunduki.
Pamoja na changamoto Lukuki katika chuo hicho ,Bundi anasema kuwa wameweza kutoa wahitimu 2,332 katika fani zote tatu za Maendeleo ya Jamii tangu kilipoanzishwa wengi wao sasa wako kazini.
Chuo kimeweza kupanda ngazi  tofauti katika utoaji wa mafunzo ambazo ni; ngazi ya Cheti, Stashahada ya juu,  Shahada ya kwanza na Stashahada ya Uzamili.

Anaendelea kutoa historia ya chuo kuwa Chuo kinajumla ya wanachuo 543 ikiwa wanawake ni 308 na wanaume 235.Kwa upande wa wahadhiri anasema  kina jumla ya wahadhiri 27, uwiano wa mhadhiri 1 kwa wanafunzi 20.

Aidha anasema Chuo kimeweza kujitangaza kwa njia mbalimbali,  kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wadau mbali mbali na  kuhuisha michezo.



Katika kukabiliana na uhaba wa maji  Chuo hicho  kimefanikiwa kujenga kisima kirefu cha maji safi na salama kwa jumuiya ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii – Tengeru tangu 2003,

Hata hivyo anasema katika kuboresha miundo mbinu ya Chuo wameweza  kujenga kumbi pacha mbili za mihadhara zilizokamilika 2008, na kugharimu shs. 668,502,611.77/= zikiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 600 kwa wakati moja.
Bunduki anasema kuwa wanaendelea  na ujenzi wa maktaba ya kisasa unaotegemewa kugharimu jumla ya shs.513,382,914/= kwa awamu ya kwanza maktaba hii ikikamilika itakuwa na uwezo wa kuhudumia wanafunzi 200 kwa wakati moja.  Kumekuwepo na tatizo la ukosefu wa fedha hivyo kuchelewesha awamu ya pili ya ujenzi

Bunduki anasema kuwa wanakabiliwa na Changamoto Lukuki baadhi ya changamoto hizo zikiwa ni  Uchakavu  wa miundo mbinu ikiwa ni  madarasa, mabweni, nyumba za watumishi na jengo la utawala,na kueleza kuwa  uongozi wa Chuo unajitahidi  kufanya ukarabati wa hatua kwa hatua hususani mabweni,  zahanati, madarasa na nyumba za watumishi ikiwa ni wakati fedha zinapatikana .

Anavunja ukimya na kueleza kuwa pamoja na kujitahidi kutoa huduma wanapata vikwazo na kufanya shughuli za chuo kusuasua ,kuwa mahitaji ya uendeshaji wa Chuo mfano  mwaka  2012/2013 ni Tshs. 5,147,758,984/-lakini fedha zinazopatikana  kutokana na mapato ya ndani ni Tshs. 691,505,600/= ruzuku ni Tshs 49,583,000/=, mishahara ni Tshs. 1,121,215,924/= sawa na asilimia 36.2 tu ya mahitaji halisi ya Chuo.
Bunduki anasema kuwa  Chuo kinajitahidi kuainisha vyanzo vingine vya mapato ikiwa ni pamoja na ada za mafunzo ya muda mfupi, utafiti na ushauri wa kitaalamu.

Akizungumzia masuala mengine anasema kuwa Chuo kinakabiliwa na uhaba  wa vyombo vya usafiri  hususani pale mafunzo ya vitendo yanapohitajika  na hata katika utendaji wa majukumu ya kila siku, na kuwa Chuo  kinakabiliwa na upungufu wa watumishi wa kada mbalimbali ikiwemo wahadhiri na watumishi waendeshaji. Na kufanya huduma ya taaluma kudorora .
Kwa upande wao  baadhi ya watumishi wa Chuo hicho wameeleza kuwa ,Maslahi duni yanawavunja moyo watumishi  katika utendaji wao wa kazi wa kila siku, kwa kuwa wanashindwa kumudu gharama za maisha zinazopanda kila wakati.

Watumishi hao wanasema kuwa wanaweza kukabiliana na matatizo hayo  ikiwa Serikali itatoa fursa ya chuo kujiendesha na kujisimamia chenyewe na mwongozo wa Utumishi kupitishwa.
Mkuu huyo anasema kuwa  matarajio ya badae ni Chuo ni kitahuisha mafunzo ya muda mfupi katika nyanja za uhamasishaji jamii, ubunifu na uandikaji wa miradi, uandikaji taarifa, uongozi, haki za Mama na Mtoto, Ujasiriamali n.k.  Pamoja na kutoa mafunzo ya muda mrefu chuo kinategemea pia kujikita katika ushauri wa kitaalamu na utafiti hususani katika masuala ya kijamii.Chuo kwa kushirikana na bodi ya Uendeshaji na Wizara,  kimepata ithibati ya kujiendesha kisheria katila utoaji wa mafunzo  (AUTONOMY).
Kwa upande wao Afisa habari wa Chuo hicho Clara Emanuel anasema kuwa Chuo kina mahusiano mazuri na vyuo vingine ,katika Nyanja ya michezo na mijadala ya taaluma ,na kuwa kupitia michezo wanafunzi wameweza kubadilishana uzoefu na kuepuka kujiingiza katika vitendo vya uhalifu

Anasema kuwa wanafunzi wengi katika Chuo hicho wamejikita katika taaluma zao ,na kuwa muda mwingi wanatumia kujisomea ,na kueleza kuwa nidhamu hiyo imetokana na uongozi bora wa chuo .

Kwa Upande wake mmoja wa watumishi katika maktaba ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii  Tengeru   Joseph Atanasi ,ambaye mwandishi wa makala hii alifanya mahojiano nayo anasema kuwa vitabu havitoshelezi na kueleza kuwa wanahitaji vitabu zaidi na bora vinavyoendana na wakati ,ikiwa ni kuwawezesha wanafunzi kusoma kulingana na wakati ,
Anasema kuwa vitabu vilivyo ni vya miaka ya nyuma na kueleza kuwa bado vinafaa kutumika lakini vitabu vipya vinahitajika kutokana nauhalisia wa karne hii ya Sayansi na Tekenolojia .
Tangu kuanzishwa kwake Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Tengeru Kiliwahi kuongozwa na wakuu wa Chuo wapatao nane( 8)kati ya hao wanawake wawili Bi. Florence Ghamunga 1985-1986 na Bi.Celina Shinyambala 1994-1998.
Mkuu wa Chuo wa kwanza aliitwa Captain E.P.Machumu na Mkuu wa Chuo wa sasa ni Bw. Anatory B.Bunduki.
Mwisho



Serikali imekipa kisogo chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru

Jengo Pekee bora Chuo cha Maendeleo Jamii Tengeru,Serikali inatia aibu ,Chuo kina miaka 45 tangu kuanzishwa 

March 25, 2013

Vijana million 2 kunufaika kupitia Michezo



Vijana ,walemavu,watoto  na Vijana  wa Tanzania ,wapatao Milion 2 watarajiwa kunufaika na Michezo

Na Mary  Mwita ,Arusha

SUALA la kuendeleza michezo hapa nchini ni la kila mtu hususani wadu wa michezo ,wenye nia dhabiti ya kukuza michezo nchini ,ikiwa  ni hatua mojawapo ya kuwezesha nchi ya Tanzania kungara katika Dunia kupitia michezo .

Harakati za kusaka wadau wa michezo kunusuru Michezo zimeanza kwa Serikali kupiga hodi katika baadhi ya Mikoa kuwasaka ikiwa ni kutaka kujua maoni yao ya jinsi ya kuboresha michezo na mazingira ya Michezo hapa nchini .

Serikali imepiga hodi katika Mkoa wa Arusha na kukutana na wadau wa Michezo kutoa Shule za Sekondari ,Vyuo na taasisi binafsi na Serikali ,kujadili namna ya kuboresha michezo  ambapo wadau wa michezo wanasema katika kunusuru Michezo lazima kiundwe  Chombo kimoja kitakacho nusuru Michezo .

Wakiwa katika warsha ya siku moja katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Wilaya ya Arusha katika jiji la Arusha wanavunja ukimya kuwa wakati umefika wa michezo kupewa kipaumbele ikiwa ni kuwezesha vijana kushiriki katika michezo kama Ajira .

Aidha kwa nyakati tofauti wanasema kuwa Tanzania inaweza kupaa katika uchumi ikiwa itangara katika michezo kwa kuwa itakuwa inaonekana katika Ramani ya dunia na kujulikana na watu na wadau wa maendeleo ya kiuchumi na michezo .

Wanasema Mazingira ya michezo ikiwa ni miundo mbinu bora haina budi kuboreshwa kuwezesha wachezaji kucheza vizuri na kushinda .

Katika harakati za kupata uhalisia wa Warsha hiyo Super Star imefanya mahojiano na Afisa Michezo Mkuu wa Wizara ya Habari ,Vijana ,Utamaduni  na Michezo  Nicolas  Bulamile  na kueleza kuwa Warsha hiyo  ina lengo la kuwezesha wadau wa Michezo Mkoa wa Arusha kuelewa rasimu ya mfumo wa Ufuatiliaji wa michezo

Bulamile anaendelea kusema kuwa sababu ya pili  kuwawezesha kujifunza na hatimaye kuwa sehemu ya ufuatiliaji wa  mfumo wa michezo  na tathimini ya maendeleo ya michezo nchini

Pia anasema kuwa kupitia warsha hiyo wadau watajifunza na kuweza kusaidia kutengeneza mfumo wa ufuatiliaji na  kutoa
tathimini  ya michezo  nchini .

Anasema kuwa matokeo ya warsha hiyo ni kuwa maoni ya wadau yatawezesha  kuboresha rasimu ya mfumo wa ufuatiliaji  na tathimini ya maendeleo ya michezo nchini ,na kuwa rasimu hiyo itaanza kufanya kazi mwezi April ,na kuwa Mikoa iliyotengwa kwa ajili ya kuanza zoezi hilo ku ni Arusha,Dar es Salaam ,Mwanza ,Ruvuma ,Mjini Magharibi,  Zanzibar.

Pamoja  na mambo mengine anasema kuwa lengo la mradi huo ni kuwezesha  na kuboresha maisha ya watoto na vijana kupitia mradi wa  International Inspiration  ambao una lengo la kufikia vijana Million 2 ,mradi unaotekelezwa baina ya Serikali ya Tanzania na Uingereza .

Bulamile anaweka bayana kuwa mradi huo ni matokeo wa utekelezaji Ahadi  ya  Nchi ya Uingereza ,wakati walivyokuwa wanaomba ridhaa ya kuwa wenyeji wa mchezo wa Olimpiki mwaka 2005 ,Singapore  ambapo nchi nyingi zilikuwa zinasaka nafasi hiyo ,lakini Uingereza ilibahatika kupata

Uingereza ilitoa ahadi ya kusaidia vijana million 12 kupitia michezo ikiwa watapata nafasi ya kuwa wenyeji wa mchezo wa Olimpiki  na walipata nafasi hiyo na wakaanza kutekeleza ahadi hiyo mwaka 2007  ikiwa wamelenga nchi zilizobainika kuwa na vigezo bora vya michezo Tanzania ikiwa mojawapo .

Kwa upande wa Afrika nchi zilizobahatika na ahadi ya Uingereza ni  Afrika Kusini ,Msumbiji ,Nigeria ,Uganda ,Tanzania ,Ethiopia ,Misri  na Mozambique.

Nchi za Ulaya zilizobahatika ni Urusi ,Ispania ,Ufaransa ,Marekani ,Marekani na kuwa miradi hiyo ilianza kutekelezwa mwaka 2007 na mradi huo unadumu kwa kipindi cha miaka 3

Afisa huyo anasema kuwa Tanzania imeanza kutekeleza mradi huo baada ya kuanisha mahitaji  ya kutekeleza mradi huo na kuwa walianisha na kutaka kuboresha Sera zinazohusiana na michezo nchini ,walianisha hitaji la kuhamasisha wanawake ,walemavu ,vijana na watoto kuhamasishwa kupenda michezo na kuongeza idadi yao katika michezo.

Aidha waliandika umuhimu wa kuongeza kuboresha elimu ya michezo katika shule . na pia Wataalam wa michezo kuendelezwa .

Anasema kuwa Serikali ya Tanzania inafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa mpango  na mradi huo unafanikiwa ,ikiwa ni kuinua kiwango cha michezo nchini ,na kuwezesha vijana kukuza vipaji vyao kupitia mpango huo.

Anahitimisha kwa kuwataka wadau wa michezo  kushiriki katika kukuza michezo  kwa kupitia mradi huu ,kwa michezo inaweza kukua ikiwa wadau wote wa michezo watashiriki na kupenda michezo.

Mwisho……………………

Afisa Habari Mkuu ,Wizara ya Habari ,Vijana ,Utamaduni na Michezo ,akitoa ufafanuzi wa nia ya kukuza michezo nchini ,wakati wa mahojiano na Mwandishi wa Makala hii

Afisa Michezo  Mkuu ,Wizara ya Habari ,Vijana ,Utamaduni na Michezo

February 7, 2013

Askofu Laizer Afariki DUNIA


Askofu wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania  dayosisi ya kaskazini kati Askofu Thomas lazier amefariki Dunia jioni ya leo.
Habari ambazo zimethibitishwa na katibu Mkuu wa dayosisi hiyo Israel Ole Karyongi zimesema kuwa askofu alikumbwa na mauiti majira ya saa  12 za jioni ya leo.
“Ni kweli baba Askofu amepita na tuko katika hali ya dharura ngumu na tungependa mtuachie nafasi ili tuwape taarifa juu ya msiba huu kesho”alisema Karyongi akizungumza kwa njia ya simu .
Askofu lazier ndiye  askofu wa kwanza wa na mwanzilishi wa dayosisi  hiyo ambayo awali ilikuwa ikiitwa dayossi Mkoani Arusha kabla ya mwaka juzi kubalishw ajina na kuitwa dayosisi ya kaskazini kati.
Ni msiba mkubwa mno katika Mkoa wa Arusha kutokana na askofu huyo  kupata umaarufu katika kazi zake za kiroho na kijamii husasan jamii ya kabila la wamasai.
Anatajwa kushiriki katika kuendeleza jamii hiyo kielimu kwa kubuni na kuanzisha shule zaidi ya ishirini za sekondari zikiwemo maalum kwa ajili ya watoto wa kike.


December 28, 2012

Rc Arusha akizungumza na wadau wa Maendeleo Meru

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mlongo akizungumza  na wananchi Meru na wadau wa Maendeleo ya Meru

Mwandishi wa Habari Mary Mwita akiwa kazini Meru


Mwandishi Mary Mwita akifanya mahojiano na bibi Kizee Meru

Mary Mwita apewa tuzo ya uandishi bora na RC ,Arusha

Mwandishi Mary Mwita ,apata tuzo la uandishi bora Meru ,pichani yupo chuo kikuu Tumaini Makumira

Serikali kunusuru Vijana Meru


 VIJANA MERU kujishindia million 10


VIJANA katika Halmashauri ya Meru wanatarajiwa kuondokana na tatizo la ajira baada ya Uongozi wa Halmashauri hiyo kupanga mpango wa kuwawezesha vijana  kupitia vikundi katika kata zao kwa kutoa million 10 kila kata ,ikiwa ni sehemu ya mapato ya Halmashauri hiyo .

Akitoa ufafanuzi wa utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika Halmashauri hiyo Afisa Mipango wa Halmasahuri hiyo Hamisi Singano aliwaambia waandishi wa habari kuwa fedha hizo zitatolewa kila mwaka kupitia vikundi vya vijana na kuwa wanatarajia kuona mabadailiko ya maendeleo kwa vijana .

Singano akitoa ufafanuzi huo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru  Nyerembe Munasa Sabi na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Meru ,Triasas Kagenzi alisema kuwa maendeleo ya haraka yanachangiwa na nguvu kazi ya vijana  na akina mama , kuwa Halmashauri hiyo imeamua kutoa kipaumbele kwa vijana na wanawake.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Nyerembe Munasa Sabi alisema kuwa  Serikali ya Chama cha Mapinduzi imefanikiwa kusaidia wananchi kufikia malengo ya mafanikio na kuwezesha wananchi wa Halmashauri hiyo kuweza kukabiliana na mazingira wanayoishi kwa kupata huduma za msingi kama vile maji ,elimu ,miundo mbinu .

Munasa  Sabi aibainisha kuwa katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maendeleo zaidi katika Halmashauri hiyo jumla ya ekari 400 katika kijiji cha Malula  limetengwa kwa ajili ya kuanzishwa mradi utakaojulikana kama Economic Proccessing zone  (EPZ)

Alisema Vijana zaidi ya 500 wanatarajiwa kupata ajira katika eneo hilo ,kwa kuwa kutakuwa ni eneo la uzalishaji na uwekezaji vitega uchumi lukuki.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri  ya Meru Triasas Kagenzi alisema kuwa kabla ya kupatiwa fedha hizo vijana watapatiwa mafunzo ya ujasirimali ili kuwawezesha kuanzisha miradi ya maendeleo na kufanikiwa .

Kagenzi alisema kuwa ikiwa vijana watajizatiti katika uzalishaji ni wazi kuwa maendeleo katika jamii yatafikiwa kwa haraka na kupunguza wimbi la wahalifu katika jamii linalotokana na ukosefu wa Ajira .

Mwisho.