June 28, 2013

Mkurugenzi TAMIHA Crispin Mugarula akizungumza na Yatima anaowalea na kuwatunza


 Mkurugenzi wa TAMIHA Crispin Mugarula  ,akizungumza na watoto Yatima anaowalea na kuwasomesha ikiwa ni kati ya watoto 194 ,wanaosoma Shule ya St.Vivian Maji ya Chai ,Arumeru ,Arusha ,shule iliyoanzishwa na Mkurugenzi huyo kwa ajili ya watoto Yatima na watoto wengine wa jamii ya Meru na Mkoa wa Arusha 


Arusha yajizatiti kutoa huduma ya Afya

Na Mary Mwita ,Arumeru

AFYA bora za watu katika jamii yeyote duniani ni  matokeo ya maendeleo kwa kutokana na ukweli kuwa nguvu kazi za watu ni muhimu katika uzalishaji ambapo watu wenye afya njema ,wanahitajika kushiriki katika shughuli husika .
Kutokana na uhalisia huo ,Halmashauri ya Arusha katika Wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha kupitia wataalam wa Afya na watendaji wa Halmashauri hiyo wanafanya kila jitihada kuhamasisha watu kujenga utamaduni wa kupima Afya zao na kubaini matatizo yanayokabili kiafya na kupata tiba mapema .
Wanawake  katika jamii hiyo wanapewa elimu kuhusu umuhimu wa kuhudhuria katik vituo vya afya hususani wakati wa ujauzito ikiwa ni kuwalinda watoto wao toka wakiwa tumboni ,kwa kupata ushauri wa kitaalam ,ikiwa ni pamoja na kuwakinga watoto dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.
Miongoni wa wananchi waliopata elimu ya afya ya uzazi na kuhimizwa kuchangia huduma ya afya ni wananchi wa Olkokola ,katika Halmashauri ya Arusha ,elimu iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Arusha  Dkt. Tobias Mkina 

Mkina mtaalam wa Afya anawataka akina mama kujenga utamaduni wa kuhudhuria Kliniki mapema ,kuepusha madhara wakati wa kujifungua .

“Akina mama ,ninawaomba sana mjenge utamaduni kwa kwenda kliniki ,kwa kuwa baadhi ya akina mama hapa ,bado wanajifungulia nyumbani kwa msaada wa wawakunga wa jadi ,ninawaomba sana ,mjali afya zenu ,msipende   kujifungulia  nyumbani ,munaweza kupata madhara ikiwa ni pamoja na kifo .”anasema Mkina

“Kwa sasa hakuna kisingizio cha ukosefu wa Hospitali ,maana kuna hii hospitali ya Oltrument iliyozinduliwa na Mheshimiwa  Rais  Jakaya Kikwete ,hivyo ninawaomba sana ,muitumie vyema kwa ajili ya kupata huduma bora za Afya .”anaongeza Mkina
Pamoja na mambo mengine anawataka wananchi wa jamii hiyo ,kuchangia huduma ya  mfuko wa  Afya  jamii  na  kuwawezesha kupata huduma ya afya kwa mwaka mzima ,ikiwa watalipa Tsh 10,000  
Halmashauri hiyo ina jumla ya vituo vya kutolea huduma za Afya  48 ,ikiwa ni Hospitali  mbili ,moja ikiwa ni Shirika la dini ambayo kwa sasa ni Hospitali Teule ya Halmashauri ya Arusha

Vituo vya afya  ni 5  ,vya Serikali  vinne  na kimoja  kinamilikiwa  na mtu binafsi ,Zahanati 41  ambazo kati ya hizo  25 ni za Seriali na 16 za Mashirika  na watu binafsi .

 Huduma  za Afya zinazotolewa ni ,Huduma za wagonjwa wan je ,Huduma za Afya ya Kinywa na meno ,Huduma ya Afya akili ,Huduma ya maabara  na damu salama ,Huduma za afya ya Uzazi  na mtoto

Nyingine ni  Huduma ya Ushauri  nasaha  na Upimaji  VVU ,Huduma  za Utoaji wa dawa za kupunguza  makali ya Virusi vya Ukimwi ,Huduma za Kifua  Kikuu na Ukoma ,Huduma za Kifua Kikuu na ukoma ,Huduma za Kulaza Wagonjwa kwa baadhi ya vituo

Akitoa ufafanuzi zaidi Dk.Mkina anasema kuwa wameipa kipaumbele huduma ya Wazee ,kuwa katika Hospitali Teule ya Selian  na Hospitali ya Oltrument   na kuwa   Robo ya mwaka Januari  hadi March 2012 ,Wazee  121,wanawake wakiwa 58 na wanaume 63

Robo ya mwaka April hadi June  2012 ,Wazee  226  wanaume 114, wanawake 112 na Robo ya mwaka Julai hadi Septemba  2012 Wazee 301  wanawake wakiwa 110 na wanaume wakiwa 191
Mganga huyo anadai kuwa huduma ya afya kwa wazee inaendelea kuboreshwa ilikuweza kunufaisha Wazee wengi zaidi .
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha ,Fidelist Lumato anasema kuwa lengo la Halmashauri hiyo ni kuona wananchi wa Halmashauri hiyo wakiwa wanapata huduma bora ya afya na kuwawezesha kushiriki katika ujenzi wa Taifa .
 Kimsingi anasema kuwa majengo bora yamejengwa katika Hospitali ya Oltrument na ambayo kwa kiasi kikubwa yameinua hadhi ya Hospitali hiyo ,na kuwa  majengo hayo ni matanao  na   yamegharimu Tshs  624,650,920.30

Anafafanua kuwa  Jengo la Upasuaji (Theatre)  Tshs  118,339,526,Wodi ya Upasuaji (Surgical ward)  Tshs 140,878,004.10 ,Maabara Tshs 22,650,012.25  ,Wodi ya wanaume 134,365,871.35,Wodi ya Wanawake  Tshs 154,751,002 .50,Ukarabati wa Majengo ya Zamani  Tshs  53,666,503 

Lumato, anasema kuwa Jengo la Upasuaji limejengwa na ufadhili wa Shirika la Umoja wa Madaktari  wa Kijerumani  la Organization for International Medical  Cooperation ( VIMZ).

Jengo la Wodi ya upasuaji limejengwa kwa ufadhili wa Umoja wa madaktari wa Kijerumani  na Halmashauri ya Arusha  ikiwa ni Tshs.55,728,004 na Tshs  85,150,000

Lumato  anasema Jengo la maabara limejengwa kwa msaada wa wafadhili wa kutoka Marekani kupitia Shirika la Centre for Disease Control(CDC) pamoja na mashine za kisasa za uchunguzi wa magonjwa mbali mbali

Anaendelea kubainisha kuwa Jengo la Wodi ya wanaume limejengwa kwa ushirikiano wa wananchi ,Halmashauri ya Wilaya ya Arusha chini ya mpango wa mfuko wa Maendeleo  ya Jamii (TASAF )  na kutokana na mapato yake ya ndani  Tshs  48,780,586 na Tshs  85,585,285.35

Mkurugenzi anasema Jengo la Wanawake limejengwa mahususi kwa ajili ya kuwalaza akina mama  na limejengwa  mahususi kwa ajili ya kuwalaza akina mama  na limejengwa kwa kutumia ruzuku  ya serikali kupitia Mpango wa Maendeleo  ya Afya ya Msingi (MMAM),na mchango wa Halmashauri kutokana na mapato ya ndani .

 Pamoja na mambo mengine anasema kuwa Hospitali hiyo  inakabiliwa na matatizo mbali mbali ikiwa ni ukosefu wa majengo muhimu yatakayokidhi mahitaji ya ongezeko la wagonjwa wa nje na kulazwa

Anataja  majengo hayo kuwa ni Jengo la Wagonjwa wa nje na Utawala (OPD),Wodi ya watoto ,Jengo la kituo cha uangalizi  na kutolea huduma kwa waathirika wa virusi vya Ukimwi,tiba  na ushauri nasaha, Jengo la X ray pamoja na mashine ya X Ray  na Jengo la kusubiria kujifungulia .
 
Kimsingi anasema  kuwa Hospitali hiyo inatarajiwa kupunguza vifo  vya watoto na wajawazito ,na kuhimiza jamii kujenga utamaduni wa kwenda katika vituo vya afya kupima afya zao ,na kuepuka kusubiri hadi mgonjwa kuzidiwa na kuwa na hali mbaya ndipo anapelekwa hospitali
Lumato anahimiza wananchi wa Halmashauri hiyo kujiunga na mfuko wa huduma ya Afya na kuchangia Tshs 10,000 ambazo mwananchi ataweza kutibiwa kwa kipindi cha mwaka mmoja pamoja na familia yake.

T
People (3)
mtanzania95



Show details

No comments:

Post a Comment