Polisi yamkamata mtuhumiwa wa mauwaji ya ukatili Jijini Arusha ,ni mwanafunzi wa Faslafa Chuo cha Kanisa Katoliki Segerea ,viungo vya marehemu vyapatikana Usa River Arusha
Na Mary Mwita,Arusha
JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha limefanikiwa kumkamata mtu
aliyetajwa kwa jina la Elijus Edward Lyatuu(31)
mkazi wa kwa tuhuma za kumnyonga
na kumua kijana Alfred Kilubahae (18) na
kukata sehemu za mwili wake wakiwa katika Hotel ya A.M Arusha
na kasha kutoweka na viungo vya marehemu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Lebaratus Sebas akizungumza
na waandishi wa Habari alisema kkuwa mtuhumiwa alikamatwa maeneo ya TRA tarehe
1/9/2015 majaira saa saba mchana
Sabas alisema kuwa mtuhumiwa amebainika kuwa ni mwanafunzi
wa mwaka wa tano katika chuo cha Falsafa kinachosimamiwa na kanisa Katoliki ,Segerea
Kamanda alisema kuwa mtuhumiwa anadaiwa kufika nyumbani kwa marehemu maarufu
kwa jina la Mandela , wiki mbili zilizopita na taarifa zinaonyesha kuwa
walikuwa na ugomvi na ni marafiki wa karibu
,lakini walishindwa kuelewana na kukubaliana kwenda kumaliza tofauti zao
hoteli ndipo mtuhumiwa alivyofanya mauaji hayo .
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha anasema mtuhumiwa
atafikishwa mahakamani kujibu
tuhuma zinazomkabili mara baada ya Polisi kukamilisha upelelizi
No comments:
Post a Comment