March 25, 2013

Vijana million 2 kunufaika kupitia Michezo



Vijana ,walemavu,watoto  na Vijana  wa Tanzania ,wapatao Milion 2 watarajiwa kunufaika na Michezo

Na Mary  Mwita ,Arusha

SUALA la kuendeleza michezo hapa nchini ni la kila mtu hususani wadu wa michezo ,wenye nia dhabiti ya kukuza michezo nchini ,ikiwa  ni hatua mojawapo ya kuwezesha nchi ya Tanzania kungara katika Dunia kupitia michezo .

Harakati za kusaka wadau wa michezo kunusuru Michezo zimeanza kwa Serikali kupiga hodi katika baadhi ya Mikoa kuwasaka ikiwa ni kutaka kujua maoni yao ya jinsi ya kuboresha michezo na mazingira ya Michezo hapa nchini .

Serikali imepiga hodi katika Mkoa wa Arusha na kukutana na wadau wa Michezo kutoa Shule za Sekondari ,Vyuo na taasisi binafsi na Serikali ,kujadili namna ya kuboresha michezo  ambapo wadau wa michezo wanasema katika kunusuru Michezo lazima kiundwe  Chombo kimoja kitakacho nusuru Michezo .

Wakiwa katika warsha ya siku moja katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Wilaya ya Arusha katika jiji la Arusha wanavunja ukimya kuwa wakati umefika wa michezo kupewa kipaumbele ikiwa ni kuwezesha vijana kushiriki katika michezo kama Ajira .

Aidha kwa nyakati tofauti wanasema kuwa Tanzania inaweza kupaa katika uchumi ikiwa itangara katika michezo kwa kuwa itakuwa inaonekana katika Ramani ya dunia na kujulikana na watu na wadau wa maendeleo ya kiuchumi na michezo .

Wanasema Mazingira ya michezo ikiwa ni miundo mbinu bora haina budi kuboreshwa kuwezesha wachezaji kucheza vizuri na kushinda .

Katika harakati za kupata uhalisia wa Warsha hiyo Super Star imefanya mahojiano na Afisa Michezo Mkuu wa Wizara ya Habari ,Vijana ,Utamaduni  na Michezo  Nicolas  Bulamile  na kueleza kuwa Warsha hiyo  ina lengo la kuwezesha wadau wa Michezo Mkoa wa Arusha kuelewa rasimu ya mfumo wa Ufuatiliaji wa michezo

Bulamile anaendelea kusema kuwa sababu ya pili  kuwawezesha kujifunza na hatimaye kuwa sehemu ya ufuatiliaji wa  mfumo wa michezo  na tathimini ya maendeleo ya michezo nchini

Pia anasema kuwa kupitia warsha hiyo wadau watajifunza na kuweza kusaidia kutengeneza mfumo wa ufuatiliaji na  kutoa
tathimini  ya michezo  nchini .

Anasema kuwa matokeo ya warsha hiyo ni kuwa maoni ya wadau yatawezesha  kuboresha rasimu ya mfumo wa ufuatiliaji  na tathimini ya maendeleo ya michezo nchini ,na kuwa rasimu hiyo itaanza kufanya kazi mwezi April ,na kuwa Mikoa iliyotengwa kwa ajili ya kuanza zoezi hilo ku ni Arusha,Dar es Salaam ,Mwanza ,Ruvuma ,Mjini Magharibi,  Zanzibar.

Pamoja  na mambo mengine anasema kuwa lengo la mradi huo ni kuwezesha  na kuboresha maisha ya watoto na vijana kupitia mradi wa  International Inspiration  ambao una lengo la kufikia vijana Million 2 ,mradi unaotekelezwa baina ya Serikali ya Tanzania na Uingereza .

Bulamile anaweka bayana kuwa mradi huo ni matokeo wa utekelezaji Ahadi  ya  Nchi ya Uingereza ,wakati walivyokuwa wanaomba ridhaa ya kuwa wenyeji wa mchezo wa Olimpiki mwaka 2005 ,Singapore  ambapo nchi nyingi zilikuwa zinasaka nafasi hiyo ,lakini Uingereza ilibahatika kupata

Uingereza ilitoa ahadi ya kusaidia vijana million 12 kupitia michezo ikiwa watapata nafasi ya kuwa wenyeji wa mchezo wa Olimpiki  na walipata nafasi hiyo na wakaanza kutekeleza ahadi hiyo mwaka 2007  ikiwa wamelenga nchi zilizobainika kuwa na vigezo bora vya michezo Tanzania ikiwa mojawapo .

Kwa upande wa Afrika nchi zilizobahatika na ahadi ya Uingereza ni  Afrika Kusini ,Msumbiji ,Nigeria ,Uganda ,Tanzania ,Ethiopia ,Misri  na Mozambique.

Nchi za Ulaya zilizobahatika ni Urusi ,Ispania ,Ufaransa ,Marekani ,Marekani na kuwa miradi hiyo ilianza kutekelezwa mwaka 2007 na mradi huo unadumu kwa kipindi cha miaka 3

Afisa huyo anasema kuwa Tanzania imeanza kutekeleza mradi huo baada ya kuanisha mahitaji  ya kutekeleza mradi huo na kuwa walianisha na kutaka kuboresha Sera zinazohusiana na michezo nchini ,walianisha hitaji la kuhamasisha wanawake ,walemavu ,vijana na watoto kuhamasishwa kupenda michezo na kuongeza idadi yao katika michezo.

Aidha waliandika umuhimu wa kuongeza kuboresha elimu ya michezo katika shule . na pia Wataalam wa michezo kuendelezwa .

Anasema kuwa Serikali ya Tanzania inafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa mpango  na mradi huo unafanikiwa ,ikiwa ni kuinua kiwango cha michezo nchini ,na kuwezesha vijana kukuza vipaji vyao kupitia mpango huo.

Anahitimisha kwa kuwataka wadau wa michezo  kushiriki katika kukuza michezo  kwa kupitia mradi huu ,kwa michezo inaweza kukua ikiwa wadau wote wa michezo watashiriki na kupenda michezo.

Mwisho……………………

No comments:

Post a Comment