VIJANA MERU kujishindia million 10
VIJANA katika Halmashauri ya Meru wanatarajiwa kuondokana na
tatizo la ajira baada ya Uongozi wa Halmashauri hiyo kupanga mpango wa
kuwawezesha vijana kupitia vikundi
katika kata zao kwa kutoa million 10 kila kata ,ikiwa ni sehemu ya mapato ya
Halmashauri hiyo .
Akitoa ufafanuzi wa utekelezaji wa Ilani ya Chama cha
Mapinduzi katika Halmashauri hiyo Afisa Mipango wa Halmasahuri hiyo Hamisi
Singano aliwaambia waandishi wa habari kuwa fedha hizo zitatolewa kila mwaka
kupitia vikundi vya vijana na kuwa wanatarajia kuona mabadailiko ya maendeleo
kwa vijana .
Singano akitoa ufafanuzi huo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya
Arumeru Nyerembe Munasa Sabi na
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Meru ,Triasas Kagenzi alisema kuwa maendeleo
ya haraka yanachangiwa na nguvu kazi ya vijana na akina mama , kuwa Halmashauri hiyo imeamua
kutoa kipaumbele kwa vijana na wanawake.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Nyerembe Munasa
Sabi alisema kuwa Serikali ya Chama cha
Mapinduzi imefanikiwa kusaidia wananchi kufikia malengo ya mafanikio na
kuwezesha wananchi wa Halmashauri hiyo kuweza kukabiliana na mazingira
wanayoishi kwa kupata huduma za msingi kama vile maji ,elimu ,miundo mbinu .
Munasa Sabi
aibainisha kuwa katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maendeleo zaidi
katika Halmashauri hiyo jumla ya ekari 400 katika kijiji cha Malula limetengwa kwa ajili ya kuanzishwa mradi
utakaojulikana kama Economic Proccessing zone
(EPZ)
Alisema Vijana zaidi ya 500 wanatarajiwa kupata ajira katika
eneo hilo ,kwa kuwa kutakuwa ni eneo la uzalishaji na uwekezaji vitega uchumi
lukuki.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru Triasas Kagenzi alisema kuwa kabla ya
kupatiwa fedha hizo vijana watapatiwa mafunzo ya ujasirimali ili kuwawezesha
kuanzisha miradi ya maendeleo na kufanikiwa .
Kagenzi alisema kuwa ikiwa vijana watajizatiti katika
uzalishaji ni wazi kuwa maendeleo katika jamii yatafikiwa kwa haraka na
kupunguza wimbi la wahalifu katika jamii linalotokana na ukosefu wa Ajira .
Mwisho.
No comments:
Post a Comment