August 28, 2015

SERIKALI KUZINGATIA USHAURI WA RIPOTI YA ESRF YA MAENDELEO YA BINADAMU



IMG_4859
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (katikati) akimlaki Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Hawa Ghasia (kushoto) mara baada ya kuwasili katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha kufungua warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP). Kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
IMG_4862
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Hawa Ghasia (kushoto) akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dk. Tausi Kida (katikati) pamoja Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kuelekea sehemu maalum ya mapumziko kabla ya kuingia katika ukumbi wa mikutano.
IMG_4869
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akifafanua jambo kuhusu warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na ESRF kwa mgeni rasmi (aliyeipa mgongo kamera) na meza kuu kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa mikutano.
IMG_4966
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh. Hawa Ghasia akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha ya uwasilishaji wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya iliyofanyika jijini Arusha katika hoteli ya Ngurdoto.
IMG_4954
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dk. Tausi Kida (katikati) pamoja Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakifuatilia kwa ukaribu hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani).
IMG_4927
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
IMG_4990
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza katika warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 na Wakuu wa mikoa, wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa mikoa iliyofanyika katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.
IMG_5217
Naibu Mkurugenzi Mkazi, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Amon Manyama akiwasilisha mada ya Mageuzi ya kiuchumi yanayoendelea: kuangalia zaidi ukaji wa uchumi wakati wa warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa kwa Wakuu wa mikoa, wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa mikoa katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.
IMG_5012
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone (kushoto) wakifuatilia kwa umakini na viongozi wenzake wakati mada mbalimbali zizokuwa zikiwasilishwa kwenye warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa Wakuu wa Mikoa, Wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa jijini Arusha.
IMG_4900
Pichani juu na chini ni Wakuu wa Mikoa, Wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa waliohudhuria warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
IMG_5009
IMG_5019
IMG_4807
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (kushoto) katika picha ukumbusho na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa (katikati) na Mkuu wa wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Queen Mlozi (kulia).
IMG_5123
Mkuu wa wilaya ya Mvomero, Betty Mkwasa (kushoto) katika picha ya ukumbusho na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema nje ya ukumbi wa mikutano Ngurdoto Mountain Lodge.
IMG_5088
Pichani juu na chini Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Hawa Ghasia na meza kuu katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa waliodhuria warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
IMG_5095
IMG_5110
Mgeni rasmi na meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF).
IMG_5077
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akiteta jambo na mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Hawa Ghasia mara baada ya zoezi la picha ya pamoja.

Na Mwandishi wetu, Arusha
SERIKALI imesema itazingatia ushauri uliotolewa katika Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania ya Mwaka 2014 iliyowasilishwa kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya katika warsha yao iliyofanyika Ngurdoto, Arusha.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh. Hawa Ghasia wakati akifungua warsha yenye lengo la kujadili na kuielewa.

Ripoti hiyo ambayo imejadiliwa kama “Mageuzi ya Kiuchumi kwa Maendeleo ya Binadamu” ilizinduliwa rasmi mwezi machi mwaka huu wa 2015 inawasilishwa kutokana na haja ya viongozi hao kutambua yaliyomo na namna ya kusonga mbele katika mipango ya baadae.

Ripoti hiyo ambayo ni matokeo ya utafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imelenga kusaidia kufahamu yaliyomo katika ripoti hiyo ili kuwawezesha viongozi hao kupata uelewa mpana juu ya dhana hii ya masuala ya Maendeleo ya Binadamu.

Warsha hiyo imewezesha na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Ghasia alisema utafiti huo umelenga kuzijengea uwezo mamlaka za mikoa na serikali za mitaa ili kuziwezesha kutoa huduma bora kwa wananchi.
Ripoti hiyo ambayo imezungumzia masuala ya mageuzi ya kiuchumi kwa Maendeleo ya Binadamu imetafakari kwa undani namna ya kufanya mageuzi ya kiuchumi katika taifa ili kuleta maendeleo ya Binadamu.

Akizungumzia maendeleo alisema mwanzoni mwa karne ya 21, mataifa mengi ya kiafrika yalitengeneza Dira za Maendeleo kuwa mwongozo wa ujenzi wa uchumi na maendeleo.

“Kwa upande wa taifa letu, Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025 inalenga katika kulifanya taifa letu kuwa nchi ya uchumi wa kati wenye kutegemea zaidi sekta ya viwanda na huduma.

“ Kwa maneno mengine, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 inalenga siyo tu katika ukuzaji wa uchumi bali kubadilisha muundo wa uchumi; kwa miaka mingi uchumi wa Taifa letu umekuwa unategemea zaidi kilimo ambacho kina tija ndogo.” alisema Ghasia.

Alisema kwamba Sera za Maendeleo ya taifa letu tangu uhuru zimekuwa zikiweka kipaumbele katika dhana ya Maendeleo ya Binadamu.
“Kwa mfano, Azimio la Arusha la mwaka 1967, ambalo liliamua taifa lifuate mfumo wa ujamaa na kujitegemea lilielekeza kwamba sera, mipango na mikakati yote lazima zizingatie uboreshwaji wa maisha ya watu kwani lengo la maendeleo ni watu.” Alisema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida akizungumzia warsha hiyo alisema kwamba utafiti huyo uliofanywa na taasisi yake uliwezekana kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Idara ya uchumi), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa serikali ya Zanzibar.

Alisema Toleo hilo la Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania ya 2014 ni toleo la kwanza nchini.

Naye Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo hapa nchini na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, alizungumzia umuhimu wa mabadiliko ya kiuchumi ili taifa liwe la kipato cha kati.

Alisema ipo haja kwa taifa hili kuhakikisha kwamba linatumia vyanzo vyake vya kifedha kubadilika kutokana na hali halisi ilivyo kwa sasa.
Aidha alisema ipo haja ya kuzingatia mipango madhubuti ya kuondoa umaskini na kulinda mazingira, mambo ambayo yapo katika mpango mkakati wa Umoja wa Mataifa wa UNDAP wa maendeleo kuanzia mwaka kesho hadi 2021.

August 27, 2015

Samia Suluhu Hassan katika Kampeni za Kuwania Ugombea Mwenza wa Urais , jijini Arusha

mgombea mwenza wa nafasi ya urais  Bi. Samia Suluhu akiwa anawahutubia wananchi wa mkoa wa Arusha katika viwanja vya Samunge vilivyopo jijini hapa
 wananchi walioudhuria katika mkutano huo 
 mgombea mwenza wa nafasi ya urais akiwa anacheza ngoma  iliyokuwa inapigwa na wamama wa chama cha mapinduzi walioudhuria mkutano huo
 Baadhi ya  makada wa CCM  ambao wamewahi kugombea nafasi ya ubunge wa jimbo la Arusha mjini na kushidwa kutokana na kura kutotosha wakiwa ndani ya mkutano huo
mgombea mwenza wa nafasi ya urais  Bi. Samia Suluhu akiwa ana mnadi mgombea ubunge jimbo la Arusha mjini  Philemon Mollel hii leo
 picha zote  na woinde shizza wa libeneke la kaskazini blog

August 24, 2015

CHADEMA Jimbo la Arumeru Mashariki yasambaratika ,Mjumbe wa Mkutano Mkuu ahamia na Vijana ACT mzalendo

Mjumbe wa Mkutano Mkuu CHADEMA Samweli Shamy aliyehama chama hicho na kuhamia ACT mzalendo kwa madai ya kunyanyaswa na kunyimwa haki yake Msingi ya kuwaletea wananchi maendeleo kupitia nafasi ya Udiwani wa Kata ya Nkwandurua ,mara baada ya kumaliza mahojiano na waandishi wa habari katika Ukumbi wa PIAZA Wilaya ya Arumeru

Mjumbe wa Mkutano mkuu CHADEMA Samweli Shammy,Arumeru Mashariki akielezea sababu za kuhama CHADEMA,



MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Taifa CHADEMA  na mwenyekiti wa Kata ya Nkwandurua Wilaya ya Arumeru  Samweli   Shami  akielzea waandishi wa habari sababu za kuhama CHADEMA akiwa  na Vijana zaidi ya 1000 wa kata ya Nkwandarua ,mkutano uliofanyika katika ukumbi PIAZA Nduruma ,Wilaya ya Arumeru.

MJUMBE WA MKUTANO CHADEMA Arumeru ,ahama na Vijana 1000 kwenda ACT Mzalendo


CHADEMA Arumeru yasambaratika ,Vijana zaidi ya 1000  wahamia ACT

Na Mary John  ,Arumeru ,Arusha

MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Taifa CHADEMA  na mwenyekiti wa Kata ya Nkwandurua Wilaya ya Arumeru  Samweli   Shami  akiwa na Vijana zaidi ya 1000 wa kata ya Nkwandarua wamehamia chama cha ACT Mzalendo kwa madai ya kunyanyaswa na kunyimwa fursa  za kutumia vipaji vyao kuwaletea wananchi  maendeleo 

Mjumbe huyo akizungumza na waandishi wa habari  kwa niaba ya Vijana wenzake katika ukumbi wa Piaza Nduruma alisema kuwa Mbunge wa Jimbo la Arumeru Joshua Nassari na Katibu wa Wilaya ,CHADEMA  wameshirikiana kuwanyanyasa Vijana wa Jimbo hilo ikiwa ni pamoja na kuwanyanganya  nafasi za kuwania nafasi za udiwani 

Bw,Shami alisema kuwa  Mbunge Nassari hakubali ushindani na kuwa hataki kuona Vijana wenye uwezo wa taaluma wakiwania nafasi mbali mbali za uongozi ili wasaidie wananchi  badala yake anaweka watu kwa nguvu ,wenye kutetea maslahi yao .

Kimsingi alisema  kuwa lengo la kujiunga na CHADEMA ilikuwa ni kuweza kupata fursa ya kutumia elimu na uwezo aliyonao ili aweze  kuwaletea wananchi maendeleo 

Shamy alisema  kuwa kitendo  cha CHADEMA  Jimbo la Arumeru Mashariki kuwakata watu wenye uwezo na waliochaguliwa katika kura za maoni ni uonevu ,na kuwa hawawezi kuendelea kuona uonevu huo na kudai kuwa wananchi na wafuasi wanamuunga mkono wamebariki  ahamie chama chochote .

Alisema kuwa amehamia chama cha ACT mzalendo na kuwa anatarajia kuwa kupitia Chama hicho atawaletea wananchi maendeleo .

Pamoja  na mambo mengine  alisema kuwa wafuasi wake na wananchi wanamuunga mkono ,wameondoka  CHADEMA na kujiunga ACT mzalendo baada ya kuchukizwa na mwenendo na vitendo vinavyofanywa ndani ya chama hicho .

Fadhili mboya  Mwenyekiti wa Vijana kata ya Nkwandurua  CHADEMA  akizungumzia hatua hiyo alisema kuwa wanachukizwa na vitendo vinavyofanywa na Mbunge Nassari na kudai kuwa wanaungana na Mjumbe wa Mkutano wa Taifa CHADEMA kuhamia ACT Wazalendo 

Mboya alikiri kuwa Mbunge Nassari ameonyesha  ubabe wa wazi kwa kuwanyima watu waliochaguliwa katika kura za maoni nafasi ya kugombea nafasi za udiwani na kuwapatia watu ambao walipata kura ndogo  kitendo walichodai kuwa ni ubakaji wa demokrasia 

Lukas Kaaya ni kiongozi mwingine ambaye amenyimwa nafasi ya kuwania nafasi ya udiwani kwa kura 61 akiwashinda wenzake wanne lakini nafasi hiyo  amepatiwa  mtu ambaye aliyepata kura ndogo na kudai kuwa anahamia chama cha NCCR Mageuzi ikiwa ni kusaka haki yake ya msingi ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Kaaya alisema kuwa wananchi wa Meru wanatambua uwezo wao na watawapatia kura ,na kusisitiza kuwa vitendo vya uonevu vinavyoendelea ndani ya CHADEMA Jimbo la Arumeru Mashariki vitaendelea kuvunja chama badala ya kuimarisha .

Vijana hao wamewataka wananchi kuwaunga mkono ,na kudai kuwa kuhama chama ni haki yao ya Msingi baada ya kuona matarajio waliyoyategemea hayajafikiwa .
Mwisho………………………………………………………………………………………………