Vijana Angalikan Tanzania wasema kutumiwa na Wenye Fedha
basi wajipanga kujiinua kiuchumi
Na Mary Mwita Arusha.
VIJANA wanatajwa kuwa ndiyo wenye nguvu ,na ambao wanaweza
kuleta mapinduzi ya maendeleo katika
jamii na Taifa kwa ujumla .
Huo ni ukweli usiopingwa
na mtu yeyote ,lakini mtihani na swali ni kuwa ni wapi vijana wapate
fursa yakuonyesha uwezo wao ikiwa hawana kipato hata cha kuanzisha mradi wa
kuku ama mahindi .
Vijana walio wengi hawana ajira ingawa wamesoma ,na wengine
hawana kipato cha kuanzisha miradi ,jambo linalowakatisha tamaa na kulazimika
kujiingiza katika vitendo vya uhalifu ikiwa ni pamoja na uvutaji bangi .
Tatizo la vijana linapaswa kupewa msukumo wa pekee wa maendeleo kwa kuwahamasisha kujiunga katika vikundi vya
maendeleo ili kuepuka kuwa tegemezi katika jamii wanazoishi .
Ni wazi kuwa migogoro mingi ya kisiasa inaongozwa na vijana
kwa kutumiwa na watu wenye nguvu ya fedha kwa kuwapatia hongo ya pombe na
sigara,ili waweze kukabiliana na maadui wa Siasa .
Ikiwa jamii na Taifa inapenda
kuona hatima ya vijana ikiwa njema ni vyema ikiwasaidia kuwapatia elimu bora ya
ujasirimali
Hata hivyo ,Tayari hata Kanisa limeona kuwa ukosefu wa ajira
kwa vijana ni kikwazo kwa vijana ,hata makanisani na kuwafanya kutumiwa na viongozi
wa Dini wasiokuwa na Hofu ya Mungu .
Vijana wa Kanisa Angalikani Tanzania yaani Jimbo ,wameona
athari ya kutumiwa na wenye fedha ,na wameeleza bayana kuwa Vijana wametumiwa
katika uchaguzi wa Maaskofu ,kwa kuhakikisha kuwa Askofu anayechaguliwa ni matakwa
ya kundi fulani .
Katika kuondoa hali hiyo wanasaka dawa ya Muarubaini ambao wamedai kuwa ni kuimarisha
uchumi wa Vijana kwa kuwahimiza kushiriki katika miradi ya maendeleo ,pamoja na
kuanzisha miradi ya uzalishaji itakayokuwa na manufaa ya haraka na kwa kundi
kubwa .
Mwenyekiti wa Vijana Angalikani Jimbo Jonson Mgimba Tanzania anasema kuwa katika
kufanikisha malengo yao wanatajia kuboresha Katiba ya Umoja wa Vijana wa
Angalikan Tanzania ,ili kuweza kuweka mambo muhimu ambao hayapo kwa ajili ya Vijana
ikiwa ni pamoja na kamati za miradi .
Kimsingi anajigamba kuwa Vijana wanaweza na kuwa wakati
wakutumiwa na wenye fedha makanisani na
Serikalini imekwisha ,kwa kuwa wamekuwa daraja la mafanikio ya watu wenye uwezo wa fedha ,na baada ya kufanikiwa wanapewa
kisogo .
Naomba kuuliza Hivi ni kweli hatuwezi kweli ?Ni jibu rahisi
sana ,tunaweza ,tunatakiwa kujiamini ,na tunaweza kufanikiwa kiuchumi kupitia
njia mbali mbali na zipo ,hivyo tujipange na tushirikiane kwa pamoja ,huku
tukiomba wadau wenye mapenzi mema kujitokeza kutusaidia .
Mwenyekiti huyo anaeleza kuwa ipo miradi Lukuki ya
Maendeleo ambayo vijana
wakiwezeshwa watafanya na kuepuka kuwa
tegemezi .
“Niwambie Vijana wenzangu sisi tunazonguvu ,hakuna jambo
tunaloweza kushindwa ikiwa tutaamua kufanya na kujituma ,na Maandiko Matakatifu
yanatamka bayana umuhimu wa Vijana ,Biblia inamuulezea Kijana ni nani ,hivyo
tuamue kwa vitendo na tuonyeshe jamii kuwa tunaweza .”anasema
Katika kuonyesha kwa vitendo Vijana hao wanalazimika
kuanzisha mchango baina yao na wadau waliohudhuria mkutano huo ,na kuweza
kupata zaidi ya Million 15 ikiwa ni ahadi na fedha taslimu .
Vijana hao wakiwa katika Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima
Morogoro yaani (WAMO) wanaeleza furaha yao kwa mgeni Rasmi katika mkutano wao
wa siku Mbili ,Askofu Stanely Hotay wa Dayosisi ya Mount Kilimanjaro kuwa
,wanajiona wenye faraja wakiona viongozi wao wakiwaunga mkono .
Wanashindwa kuficha furaha yao na kueleza kuwa Askofu huyo
amekuwa karibu na vijana wa Kanisa hilo ,na kuomba awe Mshauri wao wa karibu
kwa kuwa wameona kuwa ana nia dhabiti na Vijana.
Aidha wanamtaja mtu mwingine kuwa ni Bwana Mgaya ,ambaye
wanadai ni mtumishi wa Mungu ambaye ameona umuhimu wa Vijana na kuwasaidia
pindi walivyohitaji msaada wake.
Katika hatua nyingine wanamshukuru Askofu Mkuu wa Kanisa
hilo na Katibu Mkuu wa Kanisa hilo kwa kushiriki katika mkutano wa Vijana na
kuzungumza nao ,na kueleza kuwa wamepata nguvu ya kuendeleza mikakati ya
kujikomboa katika umaskini .
“Tunashukuru kwa michango na ushauri wenu tunaendea kufanyia
kazi ,tunaomba msichoke kutusaidia ,tunahitaji msaada wenu kama walezi ,na
marafiki wa kweli wa Vijana “.anasema
Kwa upande wake Askofu Stanely Hotay hakusita kuzungumza na
Vijana hao kuhusu kupinga maovu ,hususuani suala la ushoga ,ambalo Mataifa ya
Magharibi wamelivalia Nguja .
Hotay anasema kuwa amekuwa
ni miongoni wa Viongozi waliohudhuria mkutano wa kupinga Ushoga na
alipinga bila woga na kuvutia baadhi ya Viongozi wa Nchi za Ulaya ,na kutamani
kuzuru Tanzania ,kwa kuwa alionyesha msimamo kuwa hiyo ni dhambi na haina
uhalali wowote.
Vijana muwe tayari kukataa maovu ,na maovu mukatae wakati
wowote mchana na usiku ,lazima Mungu aheshimiwe na ninyi vijana munayo nafasi
kubwa sana kupinga kila jambo baya ,msikubali kutumiwa na watu waovu waliokata
tama ,bali kuweni kielelezo cha kuonyesha watu njia sahihi .
“Maisha na mazingira magumu yasiwafanye mukashiriki katika
maovu ,Mataifa ya Magharibi yanatuburuza kwa kutaka tufanye matakwa yake
msikubali hata kidogo ,lazima mujue kuwa mpango wao wa kuhimiza ushoga
hakuuanza leo ,walionzisha mpango huo wamechukua muda mwingi na hata kuingia
Vyuoni na kufundisha vijana watakaofanikisha malengo yao ,hivyo kuweni makini
sana ,kwa kuwa Mungu wetu hadhihakiwi “
Ni wazi kuwa hao wanaohimiza ushoga hawakuanza leo ni
mkakati wa muda mrefu wa kutenda dhambi ,walianza miaka 30 iliyopita ,na
wamefanyta hivyo katika vyuo vikuu katika nchi husika kufundisha vijana miaka 3
,ikiwa ni kuwaandaa kuhimiza ushoga na huo ni mradi wao ,hivyo vijana kuweni
macho .
Askofu Hotay akiwa ananukuu maandiko Matakatifu katika
Biblia kitabu cha Warumi 10 anawataka Vijana kuwa mstari wa mbele kupinga maovu
Vijana nawataka dhambi muitangaze mchana na wala siyo usiku
,yaani msione haya kutangaza dhambi ili
wanaotenda waache na kumfuata Mungu .
Hotay anaendelea kuwapa kiburi vijana kuwa wana nguvu na mtu
awaye yote asiudharau ujana wao ,huku akinukuu maandiko matakatifu ITimotheo
12;6
Pamoja na mambo mengine anakemea ushirikina na kudai kuwa
Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika inayoongoza kwa Ushirikina ,na kuwataka
vijana kuepuka ushirikina kwa kuwa Mungu
ni zaidi ya yote ,kwa kuwa hata hao washirikiana wanataja Mungu ,japo
hawajui ni Mungu yupi wanayemwabudu.
Askofu huyo pia anasisitiza kuwa wote waliondoka katika
Imani ya kweli wanazo njia zao
wanazofuata na kutaka vijana kusimama katika Imani na kumwamini Mungu wa kweli
,na kunukuu maandiko Matakatifu katika Biblia katika ITimotheo 1-4 kuwa kila
anayeacha imani ya kweli afuata njia zake.
Naye Askofu Mkuu wa Tanzania ,alizungumza na Vijana hao
nakuwataka kuanza sasa kujitegemea kwa kuwa ameona nia yao njema ya kujikomboa ,na kudai kuwa
Kanisa linawaunga mkono na kuwataka kuanza mchakato wa kurekebisha Katiba
mapema ,ili mabadiliko ya kiuchumi na mambo mengine ya Msingi yaweke kwenye
Katiba .
Askofu huyo kwa kuunga jitihada za Vijana mkono anaahidi
kuchangia Milion 3 kwa ajili ya mfuko wa jimbo Vijana ,na kuungwa Mkono na
Askofu Hotay anayechangia million 1.
No comments:
Post a Comment