Ukatili wa Wanawake Arumeru bado ni Tatizo ,Siku ya
wanawake yaazimishwa kwa majonzi
Na Mary Mwita ,Arumeru.
SUALA la Ukatili wa Wanawake katika Jamii mbali mbali hapa
nchini bado ni tatizo ikiwa wadau wa haki za Binadamu ,wanapigia kelele ukatili
huo.
Wilaya ya Arumeru tatizo la Ukatili wa wanawake bado nikubwa
,wanawake wananyanyaswa na wanaume zao ,wanabebeshwa jukumu la kulea familia
ikiwa ni pamoja na kusomesha watoto .
Baadhi ya wanawake wanapiga na kujeruhiwa na wanaume zao
,lakini wanashindwa kueleza ukweli kwa vyombo vya usalama kwa kuogopa
kuwajibishwa na jamii zao ikiwa watawashitaki wanaume zao .
Ingawa Siku ya wanawake
iliyofanyika tarehe 8 Machi 2014 ilifana katika maeneo mengi nchini
,lakini Arumeru hali ilikuwa yakusikitisha baada ya kupata simulizi ya jinsi
wanawake wanavyofanyiwa ukatili ,huku waathirika wa matukio wakieleza mikasa
iliyowapata .
Katika kata ya Oltruto ,tarafa ya Enaboishu,Halmashauri ya
Arusha ,Wilaya ya Arumeru ,wanawake waliangua kilio wakati mwanamke mwenzao alivyoeleza
jinsi alivyonyanyaswa na mume wake na kutelekezwa na watoto wawili .
Mwanamke huyo aliyetambulishwa kwa jina la Magreth Namnyaki
,aliwafanya wanawake wenzake wachange fedha kwa ajili ya kumsaidia mwanamke huyo .
Mgeni Rasmi katika maadhimisho wanawake katika Halmashauri
ya Arusha ,Anna Msuya ambaye ni makamu Mwenyekiti wa Halmashuri ya Arusha
,anashindwa kujizuia na kueleza hali waliyomkuta mwanamke huyo akiwa nayo .
Msuya anasema kuwa ,mwanamke huyo aliungua mikono ,na
kulazwa katika Hospitali ya Selian ,na alikuwa amezuiwa na Hospitali baada ya
kupona ili aweze kulipa deni la Million 13 alizotumia akiwa Hospitali hiyo .
“Jamani ukisikia unyama ,huyo Magreth amefanyiwa unyama
,fikiria kaungua akiwa na kwa mume wake ,Mume alivyoona kaungua ,kamtelekeza
hadi watoto ,ambao ilibidi wapelekwe kwa nyumbani kwa mwaname hii ni hatari
sana”anasema Anna Msuya
Msuya anasema kuwa Serikali ilifanya jitihada za kumsaka
mwanaume huyo ,ili akamatwe ,lakini alitoroka ,na hadi sasa hajapatikana na
kueleza kuwa akipatikana lazima atachukuliwa hatua ,kwa kumnnyanyasa ,mwanamke
huyo .
Katika kuonyesha kuwa ameguswa na mkasa huyo Msuya anaongoza
wanawake waliohudhuria maadhimisho hayo kumchangia fedha Bi Magreth ,ili ziweze kumsaidia kununulia
watoto wake chakula .
Anamchangia kiasi cha Tshs
400,000 na wanawake wa jamii ya wafugaji wanafanikiwa
kumchangia Tshs 170,000
Bi Msuya anashukuru kwa mchango ,wa akina mama kwa mwanamke
mwenzao ,na kueleza kuwa atahakikisha mwanamke huyo anaanzisha biashara ndogo ndogo
,ili aweze kusaidia watoto wake wawili
aliotelekezwa nao.
“Nawashukuru kwa moyo
wa upendo ,nitahakikisha kuwa nafuatilia maendeleo ya mwanamke huyu tukishirikiana na Diwani mwenzangu Muna Twalibu ,tunatamani tumuone Magreth akiwa anafuraha na wanawake
wengine kama yeye ,tutahakikisha kuwa anasimama “anasema Anna .
Kwa upande wake Afisa Maendeleo wa Halmashauri ya Arusha
,Wilaya ya Arumeru ,Bi Mwantumu anawaambia washiriki wa maadhimisho hayo kuwa siku
ya wanawake duniani madhumuni yake
ni kujenga ushirikiano baina ya
wanawake,kutoa nafasi kwa jamii kutafakari matatizo yanayowakabili wanawake.
Mwantumu anasema kuwa maadhimisho hayo yanalenga kuthamini
mchango wa wanawake katika Nyanja mbali mbali za kiuchumi ambao awali zilikuwa
hazithaminiwi kutokana na mila na desturi ambazo zilipuuza mwanamke.
Anasema kuwa chimbuko la maadhimisho hayo ni matokeo ya
jitihada za umoja wa mataifa na matokeo
ya mikutano ya Kimataifa kuhusu wanawake
.
Mwaka 1935 nchi za ligi ya dunia (League of Nations)zilianza
kuzungumza haki za maswala ya wanawake
kama Haki za Binadamu zinazostahili kuingizwa katika Katiba yao .
Juni mwaka 1946 Umoja wa Mataifa ulianzisha Kamisheni juu ya Hadhi ya Wanawake yenye wajumbe 15.
Hata hivyo mwaka 1947 wajumbe waliongezeka na kuwa 32 ambao
ni wajumbe kutoka Afrika walikuwa 8 ,kutoka Latin Amerika wajumbe 6,Asia wajumbe 6,Ulaya Mashariki wajumbe 6 na Ulaya Magharibi wajumbe 6.
Harakati za kumuwezesha mwanamke kuwa na haki ya kupiga
kura ulipitishwa mwaka 1952 na mwaka
1957 baraza la Umoja wa Mataifa lilipitisha mswada (Convention) wa malipo sawa
ya Ujira wa kazi sawa kati ya mwanamke
na mwanaume.
Pia mwaka1960 mswada wa kuondoa ubaguzi wa elimu kati ya
msichana na mvulana ulipitishwa na mwaka 1962 mswada wa kiwango cha umri wa
kuolewa ulippitishwa .
Mwaka 1975 ,mkutani wa 1 wa wanawake Duniani ulifanyika Mexico.Mkutano huo ulikuwa
chimbuko la mwaka wa wanawake kimataifa na kuzaliwa kwa kumbukumbu ya
kuzingatia usawa,maendeleo na amani na mfuko wa maendeleo (UNIFEM) ulianzishwa.
Mwaka 1979 mswada wa kupiga vita masuala yote ya unyanyasaji
wa wanawake (Convention on the elimination of all forms of discrimination
Against women) ulipitishwa .
Mkutano wa 11 ulifanyika Copenhagen mwaka 1980,kutathmini miaka 5 baada ya Mexico
na mwaka 1985 mkutano wa III wa
Dunia wa wanawake ulifanyika Nairobi –
Kenya-Nairobi ukiwa na lengo la kubuni mikakati ya kuendeleza wanawake kwa kuzingatia usawa wa maendeleo .
Mwaka 1995,mkutano wa IV wa wanawake ulifanyika Beijing
ambalo kuzaliwa ulingo wa Beijing unao zingatia matakwa ya wanawake katika
Usawa ,maendeleo na amani
Kutokana na miswada hiyo pamoja na mikutano iliyotajwa
,mwaka 1996 ,Umoja wa mataifa uliamua maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani
yafanyike tarehe 8 machi kila mwaka .
Tanzania inatambua umuhimu wa wanawake na haki zao hivyo
kuwekwa wazi katika Katiba ya Jamhuri ya
mwaka 1977 .
Ibara ya 9 (g)ya katiba inasisitiza “Serikali na vyombo
vyake vyote vya Umma vinatoa nafasi zilizo sawa
kwa raia wote wake kwa wanaume bila kujali rangi ,kabila ,dini ,au hali
ya mtu .
Kutokana na ukweli huo Serikali iliunda Wizara maalum ya
kushughulikia maendeleo ya jamii ,wanawake na watoto kuanzia mwaka 1990 ,Wizara hiyo ndiyo
inajukumu la kuratibu shughuli zote zinazohusiana na ulingo wa Beijing ndani na
nje ya nchi .
Mwaka 1992 sera ya wanawake katika Maendeleo Tanzania
,ilipitishwa ,ambapo mwaka 2000,sera ya maendeleo ya wanawake na jinsia ,ilipitishwa zote chini ya Wizara
ya maendeleo ya jamii wanawake na watoto .
Mwisho………………………………………………………………………
No comments:
Post a Comment