Matokeo Makubwa sasa kugharimu ajira za Watendaji ,Mulongo
aapa kuwachukulia hatua watendaji wabovu
Na Mary Mwita,Arusha .
NI jambo la
kawaida kuona viongozi wakuu wa Serikali kuzuru miradi ya maendeleo na wakati
mwingine kukemea na kutoa ushauri wa jinsi ya kutekeleza miradi hiyo hatimaye
kunufaisha walengwa ambao ni wananchi wa maeneo husika .
Baadhi ya watendaji wanapata wakati mgumu wakati miradi hiyo ikitembelewa kutokana na miradi
husika kufanya kwa kiwango cha chini ,na hivyo kuzua mjadala na misuguano baina
ya mamlaka husika
Jukumu la kuhakikisha miradi inatekelezwa katika kiwango
kinachokubalika ni la kila mdau wa maendeleo ikiwa ni pamoja na wananchi wa maeneo husika .
Mpango wa Matokeo makubwa sasa (BIG RESULT NOW) kwa sasa
ndiyo unawafanya viongozi wa Serikali kukuna vichwa ,kwa kuangalia miradi ambao
imewekwa katika mpango huo inatekelezwa na hatimaye kuharakisha maendeleo .
Miongoni mwa Viongozi hao ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magessa
Mlongo ambaye anasema kuwa ikiwa viongozi na watendaji wa Halmashauri za Wilaya
Mkoa wa Arusha watashindwa kuwajibika na kuhakikisha kuwa vipaumbele kama vile
Maji ,Elimu ,Mapato ,Kilimo Nishati
inafanikiwa kwa kiwango kikubwa ,atakuwa wakanza kuwachukulia hatua
kabla ya yeye kuchukuliwa hatua
Mlongo anasema kuwa Viongozi wanapaswa kuwa mfano katika
utekelezaji wa miradi ikiwa ni pamoja na kuandaa mashamba ya mfano katika makazi yao ili wananchi wajifunze
kutoka kwao .
Mkuu huyo anasema kuwa baadhi ya viongozi ni wavivu ,na hivyo kuwafanya wananchi kushindwa
kujifunza mema kutoka kwao,kitendo alichodai kuwa hakiwezi kuvumiliwa hata
kidogo.
“Niseme lazima tuwe mfano bora ,wa kuigwa tuwaongoze
wananchi kufikia malengo ya mafanikio ,mfano suala la kilimo katika maeneo
mbali mbali hapa Arumeru wananchi kila mwaka wanakosa mvua ,wanalima mahindi
,ifike mahali wahimizwe kulima mazao yanayostahimili ukame ,kama vile mtama na
mihogo ,waache kungangania zao moja.”anasema Mlongo
Mlongo anasema kuwa wananchi wanahitaji kuona mabadiliko ya
maisha yao ,na kuwa wataweza kuwa na maisha bora ikiwa wataongozwa kufanya
shughuli zenye manufaa zitakazo waingizia kipato na kuongeza pato la familia
yao .
“Watendaji wa
Halmashauri kwa kushirikiana na
madiwani wanajukumu kubwa la kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maendeleo kupitia
vyanzo mbali mbali vya mapato ya ndani na nje ya Halmashauri hiyo .
Mlongo katika ziara
zake alipiga hodi katika Halmashauri ya
Arusha na kufanya mazungumzo na
watendaji wakuu wa Halmashauri hiyo ,kuhusu Matokeo makubwa Sasa
Mkuu huyo anawataka watendaji hao kujipanga kuhakikisha kuwa
wanashirikiana na wananchi kuboresha sekta hizo ikiwa ni njia yakuharakisha
maendeleo na kuwapunguzia wananchi umaskini kwa kuwaondolea kero sugu .
Mkuu huyo akiwa katika Halmashauri hiyo anapata fursa ya
kuzindua gari lilonunuliwa na Halmashauri hiyo kutokana na mapato ya ndani
maalum kwa ajili ya idara ya elimu .
Mkuu huyo anataka gari hilo litumike kufuatilia maendeleo ya
elimu katika Halmashauri hiyo ikiwa ni pamoja na kufuatilia mahudhurio ya
wanafunzi na walimu katika Halmashauri hiyo .
Mara baada ya kufanya mazungumzo na watalaam hao anazuru
miradi ya maji katika Halmashauri hiyo katika baadhi ya kata na kufanya
mazungumzo na wakandarasi aliowakuta katika miradi maji
Mlongo anapata ufafanuzi wa miradi hiyo kutoka kwa Mhandisi
wa maji Bi Bahati ambaye anatoa ufafanuzi wa jinsi miradi hiyo inatekelezwa .
Aidha ziara hiyo inapambwa na viongozi wa Halmashauri ya
Arusha ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mnasa Nyerembe ,Mwenyekiti
wa Halmashauri hiyo ,Saimon Saningo ,na Makamu Mwenyekiti Anna Msuya na
watendaji wengine wa Halmashauri
Mkuu huyo anaeleza kufurahishwa na utekelezaji wa miradi
hiyo na kutaka wakandarasi hao kumaliza miradi hiyo kwa wakati ikiwa ni
kuwaondolea wananchi kero ya kusaka maji .
Mlongo anawaonya viongozi wanaokwamisha miradi ya maendeleo
katika Halmashauri ya Arusha kudai kuwa hatasita kuwachukulia hatua za kisheria
Mlongo anasema kuwa viongozi kama hao hawahitajiki katika
jamii ya watu wastaarabu wanaowatakia wananchi maendeleo .
Hata
hivyo Watendaji wa Halmashauri hiyo wanafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa
wananchi wanapata maendeleo na kuupa umaskini kisogo
Katika
kutekela kwa vitendo Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya hiyo limepitisha
bajeti ya Tshs.37,319,148,736 ikiwa ni fedha zinazotarajiwa kupatikana katika
vyanzo mbali mbali vya mapato ya ndani na nje ya Halmashauri hiyo kwa ajili ya
kutekeleza miradi ya maendeleo
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri hiyo Fidelist Lumato iliyosomwa na ,bajeti hiyo
ni ya mwaka fedha 2014-2015.
Lumato
analiambia Baraza la madiwani kuwa fedha hizo zitapatikana katika mchanganuo wa
mapato ya Halmashauri billion 2,707,659,500,Ruzuku ya fidia ya
mapato 431,083,000,ruzuku ya mishahara Tshs 27,255,089,820
,ruzuku ya matumizi mengineyo Tshs.2,720,568,000, na miradi ya maendeleo
na wafadhili Tshs 4,734,884,416 .
Anafafanua
kuwa Halmashauri hiyo inakisia kutumia Tshs.37,849,293,736 ikiwa ni matumizi ya
mishahara ,matumizi mengineyo ,michango ya Halmashauri katika miradi mbali
mbali ya maendeleo ,ruzuku ya mishahara ,matumizi mengineyo ya Ruzuku ,miradi
ya maendeleo na ruzuku .
Bwana , Lumato anasema kuwa kutokana na ukomo wa bajeti hiyo
Halmashauri imelazimika kuleta maombi maalum kwa ajili ya miradi ya vijiji
19ikiwa ni kiasi cha Tshs Billion 5,455,978,106.36
Miradi
mingine iliyoombewa fedha ni mradi wa ujenzi wa Jengo la wagonjwa wa nje (OPD)
Hospitali ya Wilaya Tshs 1,800,000,000, ujenzi wa Sekondari
Tshs.200,000,000 ,Ujenzi wa Hostel za Sekondari –maeneo ya wafugaji
Tshs.200,000,000,
Nyingine
ni ukamilishaji wa Jengo la Halmashauri Tshs.200,000,000 ,ujenzi wa Vivuko Tshs
.800,000,000 ,ujenzi wa Bwawa la kukinga maji mafuriko Tarafa ya Mukulat,pamoja
na kufanya upembuzi yakinifu wa maeneo
Baraza
hilo lilipitisha Bajeti hilo kwa sauti ya pamoja na kutaka watendaji kutekeleza
wajibu wao ikiwa ni pamoja na kutekeleza miradi ya maendeleo na kufuatilia
mapato ,ikiwa ni kuwezesha Halmashauri hiyo kupata mapato kwa wakati na
kutekeleza miradi ya maendeleo .
Mwisho………………………………………