February 7, 2013

Askofu Laizer Afariki DUNIA


Askofu wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania  dayosisi ya kaskazini kati Askofu Thomas lazier amefariki Dunia jioni ya leo.
Habari ambazo zimethibitishwa na katibu Mkuu wa dayosisi hiyo Israel Ole Karyongi zimesema kuwa askofu alikumbwa na mauiti majira ya saa  12 za jioni ya leo.
“Ni kweli baba Askofu amepita na tuko katika hali ya dharura ngumu na tungependa mtuachie nafasi ili tuwape taarifa juu ya msiba huu kesho”alisema Karyongi akizungumza kwa njia ya simu .
Askofu lazier ndiye  askofu wa kwanza wa na mwanzilishi wa dayosisi  hiyo ambayo awali ilikuwa ikiitwa dayossi Mkoani Arusha kabla ya mwaka juzi kubalishw ajina na kuitwa dayosisi ya kaskazini kati.
Ni msiba mkubwa mno katika Mkoa wa Arusha kutokana na askofu huyo  kupata umaarufu katika kazi zake za kiroho na kijamii husasan jamii ya kabila la wamasai.
Anatajwa kushiriki katika kuendeleza jamii hiyo kielimu kwa kubuni na kuanzisha shule zaidi ya ishirini za sekondari zikiwemo maalum kwa ajili ya watoto wa kike.