Na Mary
Mwita Arusha
NI Jambo
lakufurahisha kuona kuwa katika jamii ya watanzania, kuna wadau wanaotamani kuona waumini wao wanaishi maisha
bora na kuepuka kuwa omba omba ,na matamanio yao wanaunga mkono Jitihada za
Serikali za kuwajengea miundo mbinu kama vile Shule ,Viwanda na miradi mingine inayoweza kusaidia idadi
kubwa ya watu .
Miongoni mwa wadau hao ni Kanisa Agape Wuema Sanctuary Ministries
International Ltd. Tanzania ambalo kwa dhamira moja limeamua kuunga jitihada za
kuwaletea wananchi maendeleo na kukutana na Viongozi wakuu wa Nchi kuelezea nia
yao ya kujenga miundo mbinu muhimu kama vile Shule ,Hospitali ,Viwanda lengo
ikiwa ni kuwezesha wananchi na waumini wao kupata huduma za msingi .
Askofu Mkuu wa
Agape Wuema Sanctuary Ministries International Ltd ,Martini Wilson
akizungumza na mwandishi wa makala hii anasema kuwa tayari wamepata baraka kutoka Serikali za
kutekeleza miradi hiyo na kuwa wanakamilisha taratibu za kisheria ili waweze
mchakato wa kutekeleza miradi hiyo
Anasema kuwa
Serikali imesema imetoa zaidi ya
ekari zaidi 8,000 kwa Kanisa la
Agape Wema Sanctuary Ministry
International Tanzania kwa ajili ya
kujenga Shule za Sekondari ,Hospitali na
miradi ya maendeleo katika mikoa mbali mbali nchini ambapo taratibu za kisheria
zinakamilishwa ili kuanza utekelezaji wa miradi hiyo .
“Tunamshukuru
Mungu kuwa Serikali imepokea maono yetu kwa furaha na imeahidi kutupatia ekari zaidi
ya 8000,na pia imetupa baraka za kuwekeza katika maeneo tunayodhani
tunamudu kwa uwekezaji ,na sisi kama Kanisa ni kuunga mkono jitihada za
Serikali za kuwaletea wananchi maendeleo ,tukishirikiana na Kanisa mama ,lilopo
Marekani .anasema Askofu Wilson.
Askofu huyo ,anataja
miji waliyopewa Mashamba ni ,Dodoma kongwa kata ya Mkoka ekari 600 ambapo itajengwa Hospitali ya Rufaa pamoja na Chuo kikuu Utafiti masuala ya afya
Miji mingine ni Morogoro ekari 2000,Mkwawa-Iringa ekari 40 ,Dodoma Bhai ekari 600 Dodoma Nkhome
ekari 600 ,Njombe ekari 350,Mbeya
Mbarari ekari 100 kwa ajili ya kujenga Hospitali ,Rukwa ekari 400 itajengwa
hospitali ya Rufaa ,Singida ekari 130
Askofu
Wilson anasema kuwa pamoja kujenga miradi hiyo wanatajia kujenga nyumba za
watumishi wa Mungu wa kanisa hilo
zipatazo 450 lengo ikiwa ni kuwaondolea adha watumishi wa
Mungu ya kuhangaika kupanga huku wakiwa
hawana uhakika wa kipato
“Watumishi
wa Mungu wamejikuta wakiishi katika maisha magumu sana ,na ndiyo maana baadhi
wamejiingiza katika mambo ambayo ni chukizo kwa Mungu ,sisi kama kanisa tumeona
mbali na kuona hilo hitaji.
Ni wazi kuwa
watumishi wa Mungu wakiwa na maisha bora watahubiri na kukemea maovu bila woga
,na kwa kufanya hivyo maovu yatapungua katika jamii “anasema Askofu Wilson
Aidha
anasema kuwa wanatamani na wananchi
watakaoishi jirani na makanisa yao ,wapate huduma za msingi na kudai kuwa nia
yao ya kujenga miundo mbinu ,itawezesha matamanio yao ya kuona watu wanaishi maisha bora na
kuepuka kuwa omba omba .
Anawakumbusha
Viongozi wenzake wa dini kuwa pamoja na
kuhubiri neno la Mungu lazima pia wafundishe waumini wao jinsi ya kujikwamu
kiuchumi na kudai kuwa ,waumini hawawezi kusikiliza neno wakiwa wana njaa
“Kuna vitu
huwezi kukwepa mfano ,mtu anajaa unamhubiria aache maovu,mfundishe jinsi ya
kupata kipato halali ,na mbinu za kupata ndiyo upate nafasi ya kukemea
maovu,mwili unahitaji na Roho pia inahitaji ,hivyo tujisahau kuwakumbusha watu
kufanya kazi kama maandiko yanayotaka” anasema Askofu Wilson .
Pamoja na
mambo mengine anakemea maovu kwa viongozi wa dini kwa kuwataka kuwa mfano bora
wa kuigwa katika jamii kwa kuikataa dhambi ,kwa kuepuka kuifanya mfano
kujiingiza katika ushoga maana hiyo ni laana .
“Jamani
niseme kuwa maandiko ya Mungu yapo wazi ,tunaonywa kuepuka dhambi ,na kuepuka
kusababisha watu kutenda dhambi hivyo ,tujitahidi kuwahubiria mema na jinsi ya
kujikwamua katika hali ngumu ya kiuchumi na siyo ,kukemea bila kuwapa suluhisho
la shida zao “anasema
Aidha
anasema kuwa watajenga 450 ikiwa
nikuwezesha watumishi wa Mungu kuishi maisha bora na kuhudumia wananchi na
waumini wa makanisa yao .
Waziri wa
Mambo ya ndani Mwigulu Nchemba akiwa amewakilisha Serikali anakutana na watumishi wa Mungu wa Kanisa
hilo ,Jijini Arusha ,katika kata ya Kisongo
nakuzungumza nao, na kuwaeleza
kuwa Serikali inatambua umuhimu
wa taasisi za dini katika maendeleo ya nchi na kusisitiza kuwa itashirikiana nao katika kuhakikisha
kuwa nia njema ya kusaidia Serikali katika ujenzi wa miradi na vitega uchumi
inafanikiwa .
Waziri
Mwigulu pamoja na mambo mengine
anawakumbusha Viongozi hao kuendelea
kuhimiza Amani nchini na kukemea maovu nchini na kudai kuwa ,bila amani na
upendo hakuna maendeleo .
“Ndugu
Viongozi wa Dini niwapongeze kwa hatua yenu hii ya kuungana na Serikali
kuwaletea wananchi maendeleo ,Serikali inawahakikishia kuwa inatambua mchango wetu ,na msisite kuomba
ushirikiano katika jambo hili jema la kujenga miundo mbinu kwa faida ya
watanzania
Niwakumbushe kuwa amani ni jambo muhimu sana tunaomba
muendelee kuihubiri bila kuchoka kwa kuwa bila amani ,hakuna maendeleo popote duniani”anasisitiza Mwigulu
Hata hivyo
tayari huduma hiyo imepokelewa Vizuri na Viongozi wa Serikali na kwa vitendo
,ambapo Spika wa Bunge Job Ndugai tayari
amekutana Timu ya Watumishi wa Mungu wakiongozana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Agape mjini Dodoma na kufanya nao mazungumzo, na
kuwapatia Baraka za kujenga katika Mji huo miundo mbinu ya Afya na Elimu .
Spika wa
Bunge la Tanzania akizungumza na Viongozi hao wa Agape anasema kuwa Serikali
inadhamini sana ,michango ya Taaasisi binafsi ikiwemo za Dini ,na kuwa Serikali
inahitaji kuungwa mkono katika kuhakikisha inafikia malengo ya kuwaletea
wananchi wao maendeleo .
“Niseme
kuwa kama Serikali ,tunasikia furaha
tukiungwa mkono katika maendeleo ,niseme kuwa mimi binafsi nimepokea taarifa
hizi kwa furaha ,natarajia kuwa wananchi watanufaika na huduma hizo pindi
zitakavyokamilika .”anasema Ndugai
Waumini na
wananchi Jijini Arusha wanaeleza kuwa hatua ya Agape kujenga miundo mbinu kwa ajili ya wananchi na Viongozi wa Dini
itakuwa imefungua ukurasa mpya wa Viongozi wa Dini kuishi maisha bora na
kuepuka kuwa tegemezi kwa waumini wao ,ambao wengi ni maskini .
Paulina
Jackob ni mkazi wa Majengo ,Jijini Arusha anasema kuwa kwa miaka mingi
watumishi wa Mungu wameishi maisha ya taabu na kuwa ikiwa watawezeshwa
kujengewa makazi bora ,wataweza kuhubiri neno la Mungu kwa uhuru bila
kishawishi .
“Mimi niseme
kuwa nimefurahishwa na huduma hii ,Mungu awasaidie wafanikishe kwa kweli mbali
na kuunga jitihada za Serikali mkono itasaidia watu na Viongozi wa dini
kukabiliana na mazingira wanayoishi,niwapongeze sana”anasema Bi Jackob
Frank Emanuel
mkazi wa Sanawari akizungumzia hatua hiyo anasema kuwa amebarikiwa na mpango
huo na kudai kuwa anatamani aone utekelezaji wake.
“Agape kweli
kama wanamaanisha wanachokisema Mungu
awawezeshe maana,kwa kweli bado tunahitaji huduma za msingi katika jamii
,na hali yetu ya kipato ni ngumu ,tukipata watu wakatujengea huduma za msingi
,tunaepukana na michango katika maeneo ya makazi yetu ,hivyo ni jambo zuri “anasema Emanuel .
Kanisa la Agape Wuema Sanctuary Ministries
International Ltd. Tanzania limefanikiwa kuwa na matawi mpaka Zanzibar
na mpango wa kujenga miundo mbinu hiyo utafikia katika maeneo yalipo matawi yake
na maeneo mengine nchini .
Mwisho