Vijana
,walemavu,watoto na Vijana wa Tanzania ,wapatao Milion 2 watarajiwa
kunufaika na Michezo
Na Mary Mwita ,Arusha
SUALA la
kuendeleza michezo hapa nchini ni la kila mtu hususani wadu wa michezo ,wenye
nia dhabiti ya kukuza michezo nchini ,ikiwa
ni hatua mojawapo ya kuwezesha nchi ya Tanzania kungara katika Dunia
kupitia michezo .
Harakati za kusaka wadau wa michezo kunusuru Michezo
zimeanza kwa Serikali kupiga hodi katika baadhi ya Mikoa kuwasaka ikiwa ni
kutaka kujua maoni yao ya jinsi ya kuboresha michezo na mazingira ya Michezo
hapa nchini .
Serikali imepiga hodi katika Mkoa wa Arusha na kukutana na
wadau wa Michezo kutoa Shule za Sekondari ,Vyuo na taasisi binafsi na Serikali
,kujadili namna ya kuboresha michezo
ambapo wadau wa michezo wanasema katika kunusuru Michezo lazima
kiundwe Chombo kimoja kitakacho nusuru
Michezo .
Wakiwa katika warsha ya siku moja katika Ukumbi wa Mikutano
wa Mkuu wa Wilaya ya Arusha katika jiji la Arusha wanavunja ukimya kuwa wakati
umefika wa michezo kupewa kipaumbele ikiwa ni kuwezesha vijana kushiriki katika
michezo kama Ajira .
Aidha kwa nyakati tofauti wanasema kuwa Tanzania inaweza kupaa
katika uchumi ikiwa itangara katika michezo kwa kuwa itakuwa inaonekana katika
Ramani ya dunia na kujulikana na watu na wadau wa maendeleo ya kiuchumi na
michezo .
Wanasema Mazingira ya michezo ikiwa ni miundo mbinu bora
haina budi kuboreshwa kuwezesha wachezaji kucheza vizuri na kushinda .
Katika harakati za kupata uhalisia wa Warsha hiyo Super Star
imefanya mahojiano na Afisa Michezo Mkuu wa Wizara ya Habari ,Vijana
,Utamaduni na Michezo Nicolas Bulamile
na kueleza kuwa Warsha hiyo ina
lengo la kuwezesha wadau wa Michezo Mkoa wa Arusha kuelewa rasimu ya mfumo wa
Ufuatiliaji wa michezo
Bulamile anaendelea kusema kuwa sababu ya pili kuwawezesha kujifunza na hatimaye kuwa sehemu
ya ufuatiliaji wa mfumo wa michezo na tathimini ya maendeleo ya michezo nchini
Pia anasema kuwa kupitia warsha hiyo wadau watajifunza na
kuweza kusaidia kutengeneza mfumo wa ufuatiliaji na kutoa
tathimini ya
michezo nchini .
Anasema kuwa matokeo ya warsha hiyo ni kuwa maoni ya wadau
yatawezesha kuboresha rasimu ya mfumo wa
ufuatiliaji na tathimini ya maendeleo ya
michezo nchini ,na kuwa rasimu hiyo itaanza kufanya kazi mwezi April ,na kuwa
Mikoa iliyotengwa kwa ajili ya kuanza zoezi hilo ku ni Arusha,Dar es Salaam
,Mwanza ,Ruvuma ,Mjini Magharibi,
Zanzibar.
Pamoja na mambo
mengine anasema kuwa lengo la mradi huo ni kuwezesha na kuboresha maisha ya watoto na vijana
kupitia mradi wa International
Inspiration ambao una lengo la kufikia
vijana Million 2 ,mradi unaotekelezwa baina ya Serikali ya Tanzania na Uingereza
.
Bulamile anaweka bayana kuwa mradi huo ni matokeo wa
utekelezaji Ahadi ya Nchi ya Uingereza ,wakati walivyokuwa
wanaomba ridhaa ya kuwa wenyeji wa mchezo wa Olimpiki mwaka 2005 ,Singapore ambapo nchi nyingi zilikuwa zinasaka nafasi
hiyo ,lakini Uingereza ilibahatika kupata
Uingereza ilitoa ahadi ya kusaidia vijana million 12 kupitia
michezo ikiwa watapata nafasi ya kuwa wenyeji wa mchezo wa Olimpiki na walipata nafasi hiyo na wakaanza
kutekeleza ahadi hiyo mwaka 2007 ikiwa
wamelenga nchi zilizobainika kuwa na vigezo bora vya michezo Tanzania ikiwa
mojawapo .
Kwa upande wa Afrika nchi zilizobahatika na ahadi ya
Uingereza ni Afrika Kusini ,Msumbiji
,Nigeria ,Uganda ,Tanzania ,Ethiopia ,Misri
na Mozambique.
Nchi za Ulaya zilizobahatika ni Urusi ,Ispania ,Ufaransa
,Marekani ,Marekani na kuwa miradi hiyo ilianza kutekelezwa mwaka 2007 na mradi
huo unadumu kwa kipindi cha miaka 3
Afisa huyo anasema kuwa Tanzania imeanza kutekeleza mradi
huo baada ya kuanisha mahitaji ya
kutekeleza mradi huo na kuwa walianisha na kutaka kuboresha Sera zinazohusiana
na michezo nchini ,walianisha hitaji la kuhamasisha wanawake ,walemavu ,vijana
na watoto kuhamasishwa kupenda michezo na kuongeza idadi yao katika michezo.
Aidha waliandika umuhimu wa kuongeza kuboresha elimu ya
michezo katika shule . na pia Wataalam wa michezo kuendelezwa .
Anasema kuwa Serikali ya Tanzania inafanya kila jitihada
kuhakikisha kuwa mpango na mradi huo
unafanikiwa ,ikiwa ni kuinua kiwango cha michezo nchini ,na kuwezesha vijana kukuza
vipaji vyao kupitia mpango huo.
Anahitimisha kwa kuwataka wadau wa michezo kushiriki katika kukuza michezo kwa kupitia mradi huu ,kwa michezo inaweza
kukua ikiwa wadau wote wa michezo watashiriki na kupenda michezo.