September 5, 2016

Agape kupewa zaidi ya ekari 8,000 na Serikali





Na Mary Mwita Arusha
NI Jambo lakufurahisha kuona kuwa katika jamii ya watanzania, kuna wadau  wanaotamani kuona waumini wao wanaishi maisha bora na kuepuka kuwa omba omba ,na matamanio yao wanaunga mkono Jitihada za Serikali za kuwajengea miundo mbinu kama vile Shule ,Viwanda  na miradi mingine inayoweza kusaidia idadi kubwa ya watu .
 Miongoni mwa wadau hao ni Kanisa  Agape Wuema Sanctuary Ministries International Ltd. Tanzania ambalo kwa dhamira moja limeamua kuunga jitihada za kuwaletea wananchi maendeleo na kukutana na Viongozi wakuu wa Nchi kuelezea nia yao ya kujenga miundo mbinu muhimu kama vile Shule ,Hospitali ,Viwanda lengo ikiwa ni kuwezesha wananchi na waumini wao kupata huduma za msingi .
 Askofu Mkuu wa  Agape Wuema Sanctuary Ministries International Ltd ,Martini Wilson akizungumza na mwandishi wa makala hii anasema kuwa  tayari wamepata baraka kutoka Serikali za kutekeleza miradi hiyo na kuwa wanakamilisha taratibu za kisheria ili waweze mchakato wa kutekeleza miradi hiyo
 Anasema kuwa  Serikali  imesema imetoa zaidi ya ekari  zaidi 8,000 kwa Kanisa la Agape  Wema Sanctuary Ministry International Tanzania  kwa ajili ya kujenga  Shule za Sekondari ,Hospitali na miradi ya maendeleo katika mikoa mbali mbali nchini ambapo taratibu za kisheria zinakamilishwa ili kuanza utekelezaji wa miradi hiyo  .
“Tunamshukuru Mungu kuwa Serikali imepokea maono yetu kwa furaha na imeahidi kutupatia ekari  zaidi  ya 8000,na pia imetupa baraka za kuwekeza katika maeneo tunayodhani tunamudu kwa uwekezaji ,na sisi kama Kanisa ni kuunga mkono jitihada za Serikali za kuwaletea wananchi maendeleo ,tukishirikiana na Kanisa mama ,lilopo Marekani .anasema Askofu Wilson.
Askofu  huyo ,anataja  miji waliyopewa  Mashamba ni  ,Dodoma kongwa  kata ya Mkoka ekari 600 ambapo itajengwa  Hospitali ya Rufaa  pamoja na  Chuo kikuu Utafiti masuala ya afya    
 Miji mingine ni Morogoro  ekari 2000,Mkwawa-Iringa  ekari 40 ,Dodoma Bhai  ekari 600   Dodoma Nkhome ekari 600  ,Njombe ekari 350,Mbeya Mbarari ekari 100 kwa ajili ya kujenga Hospitali ,Rukwa ekari 400 itajengwa hospitali ya Rufaa ,Singida ekari   130
Askofu Wilson anasema kuwa pamoja kujenga miradi hiyo wanatajia kujenga nyumba za watumishi wa Mungu wa kanisa hilo  zipatazo   450  lengo ikiwa ni kuwaondolea adha watumishi wa Mungu ya kuhangaika kupanga  huku wakiwa hawana uhakika wa kipato
“Watumishi wa Mungu wamejikuta wakiishi katika maisha magumu sana ,na ndiyo maana baadhi wamejiingiza katika mambo ambayo ni chukizo kwa Mungu ,sisi kama kanisa tumeona mbali na kuona hilo hitaji.
Ni wazi kuwa watumishi wa Mungu wakiwa na maisha bora watahubiri na kukemea maovu bila woga ,na kwa kufanya hivyo maovu yatapungua katika jamii “anasema Askofu Wilson 
Aidha anasema kuwa wanatamani  na wananchi watakaoishi jirani na makanisa yao ,wapate huduma za msingi na kudai kuwa nia yao ya kujenga miundo mbinu ,itawezesha matamanio  yao ya kuona watu wanaishi maisha bora na kuepuka kuwa omba omba .
Anawakumbusha Viongozi wenzake wa dini kuwa  pamoja na kuhubiri neno la Mungu lazima pia wafundishe waumini wao jinsi ya kujikwamu kiuchumi na kudai kuwa ,waumini hawawezi kusikiliza neno wakiwa wana njaa
“Kuna vitu huwezi kukwepa mfano ,mtu anajaa unamhubiria aache maovu,mfundishe jinsi ya kupata kipato halali ,na mbinu za kupata ndiyo upate nafasi ya kukemea maovu,mwili unahitaji na Roho pia inahitaji ,hivyo tujisahau kuwakumbusha watu kufanya kazi kama maandiko yanayotaka” anasema Askofu Wilson .
Pamoja na mambo mengine anakemea maovu kwa viongozi wa dini kwa kuwataka kuwa mfano bora wa kuigwa katika jamii kwa kuikataa dhambi ,kwa kuepuka kuifanya mfano kujiingiza katika ushoga maana hiyo ni laana .
“Jamani niseme kuwa maandiko ya Mungu yapo wazi ,tunaonywa kuepuka dhambi ,na kuepuka kusababisha watu kutenda dhambi hivyo ,tujitahidi kuwahubiria mema na jinsi ya kujikwamua katika hali ngumu ya kiuchumi na siyo ,kukemea bila kuwapa suluhisho la shida zao “anasema
Aidha anasema kuwa watajenga  450 ikiwa nikuwezesha watumishi wa Mungu kuishi maisha bora na kuhudumia wananchi na waumini wa makanisa yao .
Waziri wa Mambo ya ndani Mwigulu Nchemba akiwa amewakilisha Serikali   anakutana na watumishi wa Mungu wa Kanisa hilo ,Jijini Arusha ,katika kata ya Kisongo  nakuzungumza nao, na kuwaeleza  kuwa  Serikali inatambua umuhimu wa taasisi za dini katika maendeleo ya nchi na kusisitiza  kuwa itashirikiana nao katika kuhakikisha kuwa nia njema ya kusaidia Serikali katika ujenzi wa miradi na vitega uchumi inafanikiwa  .
Waziri Mwigulu  pamoja na mambo mengine anawakumbusha  Viongozi hao kuendelea kuhimiza Amani nchini na kukemea maovu nchini na kudai kuwa ,bila amani na upendo hakuna maendeleo .
“Ndugu Viongozi wa Dini niwapongeze kwa hatua yenu hii ya kuungana na Serikali kuwaletea wananchi maendeleo ,Serikali inawahakikishia kuwa  inatambua mchango wetu ,na msisite kuomba ushirikiano katika jambo hili jema la kujenga miundo mbinu kwa faida ya watanzania
Niwakumbushe  kuwa amani ni jambo muhimu sana tunaomba muendelee kuihubiri bila kuchoka kwa kuwa bila amani ,hakuna maendeleo  popote duniani”anasisitiza Mwigulu
Hata hivyo tayari huduma hiyo imepokelewa Vizuri na Viongozi wa Serikali na kwa vitendo ,ambapo  Spika wa Bunge Job Ndugai  tayari  amekutana Timu ya Watumishi wa Mungu wakiongozana  na Askofu Mkuu wa Kanisa la Agape   mjini Dodoma na kufanya nao mazungumzo, na kuwapatia Baraka za kujenga katika Mji huo miundo mbinu ya Afya  na Elimu  .
Spika wa Bunge la Tanzania akizungumza na Viongozi hao wa Agape anasema kuwa Serikali inadhamini sana ,michango ya Taaasisi binafsi ikiwemo za Dini ,na kuwa Serikali inahitaji kuungwa mkono katika kuhakikisha inafikia malengo ya kuwaletea wananchi wao maendeleo .
“Niseme kuwa  kama Serikali ,tunasikia furaha tukiungwa mkono katika maendeleo ,niseme kuwa mimi binafsi nimepokea taarifa hizi kwa furaha ,natarajia kuwa wananchi watanufaika na huduma hizo pindi zitakavyokamilika .”anasema Ndugai
Waumini na wananchi Jijini Arusha wanaeleza kuwa hatua ya Agape kujenga miundo mbinu  kwa ajili ya wananchi na Viongozi wa Dini itakuwa imefungua ukurasa mpya wa Viongozi wa Dini kuishi maisha bora na kuepuka kuwa tegemezi kwa waumini wao ,ambao wengi ni maskini .
Paulina Jackob ni mkazi wa Majengo ,Jijini Arusha anasema kuwa kwa miaka mingi watumishi wa Mungu wameishi maisha ya taabu na kuwa ikiwa watawezeshwa kujengewa makazi bora ,wataweza kuhubiri neno la Mungu kwa uhuru bila kishawishi .
“Mimi niseme kuwa nimefurahishwa na huduma hii ,Mungu awasaidie wafanikishe kwa kweli mbali na kuunga jitihada za Serikali mkono itasaidia watu na Viongozi wa dini kukabiliana na mazingira wanayoishi,niwapongeze sana”anasema Bi Jackob
Frank Emanuel mkazi wa Sanawari akizungumzia hatua hiyo anasema kuwa amebarikiwa na mpango huo na kudai kuwa anatamani aone utekelezaji wake.
“Agape kweli kama wanamaanisha wanachokisema Mungu  awawezeshe maana,kwa kweli bado tunahitaji huduma za msingi katika jamii ,na hali yetu ya kipato ni ngumu ,tukipata watu wakatujengea huduma za msingi ,tunaepukana na michango katika maeneo ya makazi yetu ,hivyo ni jambo zuri  “anasema Emanuel .
Kanisa  la Agape Wuema Sanctuary Ministries International Ltd. Tanzania limefanikiwa kuwa na matawi  mpaka  Zanzibar na mpango wa kujenga miundo mbinu hiyo utafikia katika maeneo yalipo  matawi yake  na maeneo mengine nchini .
Mwisho



Spika wa Bunge la Jamhuri akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Dini wa Kanisa la Agape baada ya kufanya nao mazungumzo na kukabithi ekari 600

Spika wa Bunge Job Ndugai akiwa  katika picha ya pamoja na Askofu Mkuu  wa Kanisa la Agape WEUMA  Martin Wilson  akiwa ameambatana na Maaskofu  na Viongozi wengine wa  kanisa hilo ,mjini Dodoma walipokabithiwa ekari  600 kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu Dodoma

Kanisa la AGAPE kujenga Hospitali ya Rufaa Dodoma ,yapewa ekari 600

Askofu Mkuu  wa Agape WEUMA Tanzania Wilson Martin akipokea hati ya makabidhiano ya ekari 600 kutoka kwa Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,ambapo kanisa hilo litajenga  Hospitali ya Rufaa na Chuo kikuu cha utafiti wa Afya katika mji wa Dodoma ikiwa ni kuu kuunga mkono jitihada za Serikali

AGAPE WEUMA yapewa ekari zaidi ya 8,000 na Serikali ya Tanzania

Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai akikabidhi hati ya shamba la ekari 600 kwa Askofu wa Kanisa la Agape WEUMA Tanzania,walipokutana na Timu ya Viongozi Jijini Dodoma ,Agape WEUMA Tanzania kwa kushirikiana na Kanisa Mama nchini Marekani  linatarajia kujenga miundo mbinu katika maeneo mbali mbali nchi ambapo kuna matawi yake ya Kanisa .,Serikali imewapa zaidi ya ekari   elfu  8000